Na Mwandishi Wetu, Handeni
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’
jana wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wao Yahaya Ally Khamis,
aliyeibuka na ushindi katika droo ya 15, iliyochezeshwa juzi Jumapili, huku
akitokea wilayani Handeni, mkoani Tanga. Makabidhiano hayo yamefanyika wilayani hapa katika tawi la
benki ya NMB, wilayani Handeni, mkoani Tanga, tayari kwa kuziingiza katika
matumizi ya kumkwamua kiuchumi.
Meneja
Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao
wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis kulia. Makabidhiano hayo
yalifanyika katika tawi la benki ya NMB, wilayani Handeni mkoani Tanga
jana. Kushoto ni afisa wa NMB, wilayani Handeni akishuhudia makabidhiano
hayo.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope
Heaven, alisema mchezo wao ni rahisi kucheza na kushinda, tofauti na michezo
mingine inayotumia akili nyingi pamoja na uzoefu wa kufuatilia mambo mengi ya
kukuletea ushindi. Alisema Biko ili mtu ashinde ni kufanya muamala kwenye simu
yake ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuanzia Sh 1,000 na kuendelea
ambapo namba ya kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ikiwa ni 2456, huku
mchezaji akiwa haulizwi swali lolote kwenye simu yake.
Mshindi
wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yahaya Ally Khamis, akiwa katika uso wa
furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la benki ya NMB,
wilayani Handeni, mkoani Tanga jana, baada ya kuibuka na ushindi katika
droo.
“Biko hatuulizi mtu swali lolote na ndio maana zaidi ya mtu
kufanya muamala ambao Sh 1,000 yake itampatia nafasi ya ushindi wa papo kwa
hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni
1,000,000 zinazolipwa kwenye simu mara baada ya kupokea ujumbe wa ushindi, huku
nafasi nyingine ikiwa ni kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 20
ambayo Jumapili iliyopita tulimpata Khamis tuliyomkabidhi leo fedha zake.
“Tumefarijika kuja Handeni kumpatia fedha zake mshindi wetu,
huku tukiwaasa Watanzania wote kujitokeza kwa wingi kucheza Biko kwa sababu ni
mchezo unaotoa ushindi mzuri na haraka, hivyo chezeni kwa wingi na mara nyingi
zaidi ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi,” Alisema Heaven.
Naye Khamis alisema amekuwa mchezaji mzuri wa bahati nasibu
ya Biko, jambo ambalo limemfurahisha kwa kiasi kikubwa baada ya kupata ushindi
sambamba na kupelekewa fedha zake wilayani Handeni ambako ndiko shughuli zake
za kilimo anakoendelea nako.
“Wakati napokea simu ya ushindi kutoka Biko hakika nilishusha
pumzi na kumshukuru Mungu, maana pamoja na mambo mengine ya kimaisha ambayo
nakusudia kuyafanya, lakini pia Sikukuu hii kwangu naisherehekea kwa shangwe ya
aina yake baada ya kukabidhiwa fedha zangu,” Alisema.
Baada ya kukabidhiwa fedha hizo, mshindi mwingine wa Biko wa
Sh Milioni 20 anatarajiwa kupatikana kesho Jumatano na Jumapili ijayo ikiwa ni
mwendelezo wa kutoa mamilioni ya fedha kwa washindi wao wanaopatikana kwa
kucheza bahati nasibu ya Biko, huku mwezi pekee wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500
kwa washindi ikiwa ni mwelekeo mzuri wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment