Na Mwandishi Wetu, Mbeya
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’,
leo wamemkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wao wa droo ya 18, Linda Mhewa, ambaye
ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji University (TEKU), kilichopo
jijini Mbeya.
Mshindi wa droo ya 18 ya Biko, Linda Mhewa, akiwa anazishangaa fedha zake kiasi cha Sh Milioni 20 alizokabidhiwa na waendeshaji wa bahati nasibu hiyo ya Biko Tanzania, leo jijini Mbeya.
Mwanafunzi huyo ambaye ni msichana wa pili kufanikiwa kuzoa
mamilioni ya Biko kupitia bahati nasibu ya Biko, aling’ara katika droo ya Jumatano
iliyopita, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kumwaga mamilioni kwa
kupitia mchezo wao unaotoa zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000,
20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, bila kusahau droo kubwa ya
Jumatano na Jumapili ya Sh Milioni 20.
Mkuu wa wilaya ya Mbeya, Paul William Ntinika mwenye suti, akimpongeza
mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Linda Mhewa, aliyeibuka kidedea katika droo
ya 18 iliyochezeshwa Jumatano iliyopita. Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Mbeya. Kushoto aliyeshika kipaza sauti ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope
Heaven. Kulia ni Afisa wa Benki ya NMB, jijini Mbeya. Picha na Mpigapicha wetu Mbeya.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mhewa aliyetangazwa
kuwa mshindi wa donge nono la Milioni 20, alisema kwamba ni furaha yake kuona
Mungu amemchagua katika bahati nasibu hiyo inayotikisa hapa nchini tangu
kuanzishwa kwake.
Alisema amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku akiamini kuwa
kushinda kwake ni sehemu ya kubadilisha maisha yake kiuchumi jambo ambalo ndilo
alilokusudia kiasi cha kuamua kucheza Biko.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kushoto, akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wao Linda Mhewa wa pili kutoka kushoto.
“Wakati napigiwa simu na Kajala sijaamini kabisa, nikaamini
baada ya kuona ni kweli hususan baada ya kukabidhiwa fedha zangu ikiwa ni matokeo
ya kucheza kwangu Biko, huku ukiwa mchezo rahisi kwa sababu kwa kutumia simu za
mikononi za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money kwa kuingiza namba ya kampuni 505050
na ile ya kumbukumbu 2456, huku kianzio cha kucheza kikianzia Sh 1,000 na
kuendelea,” Alisema Mhewa.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alimpongeza
mshindi wao wa jijini Mbeya, huku akimtaka ahakikishe kuwa uchumi wake unakua
kwa kuhakikisha kwamba anazitumia vyema fedha alizoshinda kutoka kwenye bahati
nasibu yao.
“Ni jambo zuri kuinuka kiuchumi kwa kupitia mchezo huu wa
kubahatisha wa Biko, ambapo tumeshuhudia mamia ya Watanzania wakiibuka kidedea
katika droo za wiki pamoja na ushindi wa papo kwa hapo unaotoka kila dakika,”
Alisema.
Kwa mwezi Mei pekee, zaidi ya Sh Milioni 500 zimetolewa kwa
washindi, huku donge nono la Sh Milioni 20 likienda kwa washindi wawili kwa
droo ya Jumatano na Jumapili.
.
No comments:
Post a Comment