Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MJASIRIAMALI mdogo wa Mlandizi, mkoani Pwani, Elisiana
Laizer, leo ametangazwa kuwa mshindi wa droo ya 19 ya kuwania Sh Milioni 20
zinazotolewa na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’,
inayoendelea kutikisa hapa nchini.
Droo ya kumpata mwanadada huyo ilichezeshwa jana jijini Dar
es Salaam na balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na mwakilishi wa
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehus Ngolo.
Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja
alisema kwamba ni furaha yake kuona droo tatu kati ya 19 zilizoendeshwa na Biko
zimewapata wanawake watatu, jambo linaloonyesha kwamba mchezo wao umekuwa wa
Watanzania wote.
“Ni jambo la kutia moyo kuona droo ya 19 imempata dada wa
Mlandizi, Elisiana ambaye anajishughulisha na biashara ndogo ndogo maeneo ya
Mlandizi, mkoani Pwani, nikiamini kuwa ni hatua nzuri kwake na Kwa Watanzania
wote wanaocheza Biko,” Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba
Biko imezidi kukolea baada ya kutoka Dodoma, ikaenda Mbeya sasa imetua mkoani
Pwani kwa mshindi wao Elisiana ambaye ameibuka kidedea kwa Sh Milioni 20, huku
zawadi mbalimbali za Biko za hapo kwa hapo zikianzia Sh 5,000, 10,000, 20,000,
50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.
“Tumetoka Mbeya juzi kwa ajili ya kumkabidhi mshindi wetu
Linda Mhewa Sh Milioni 20 zake, huku leo tukimpata msichana mwingine anayeishi
Mlandizi, mkoani Pwani aliyecheza Biko mchezo rahisi unaochezwa kwa ujumbe wa
simu za mikononi wa Tigo Pesa, M-pesa na Airtel Money, ambapo namba yetu ya
kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Jehud Ngolo, alisema Biko ni mchezo rahisi wa ujumbe mfupi wa maandishi unaotoa
ushindi kwa Watanzania wote, hivyo Watanzania wachangamkie fursa.
“Biko ni mchezo unaofuata sheria, kanuni na taratibu zote,
hivyo tunaomba Watanzania wacheze kwa wingi ili wavune mamilioni ya zawadi
kutoka kwenye mchez huu,” Alisema.
Hadi sasa tayari zimeshafanyika droo 19 za kutoa ushindi
mkubwa wa Sh Milioni 20, huku Biko wakitoa zaidi ya Sh Milioni 500 kwa Mwezi
Mei pekee tangu mchezo huo wa kubahatisha ulipoasisiwa nchini Tanzania na kutoa
fursa ya utajiri kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment