*Issa naye achota Mil 10 zake
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imezidi kushika
kasi baada ya droo yake ya 27 kutua kwa Viane Kundi wa mjini Iringa, nchini
Tanzania aliyevuna jumla ya Sh Milioni 20, huku Ally Issa Kumburu mkazi wa
Mwananyamala, jijini Dar es Salaam naye akivuna Sh Milioni 10 za Tamasha la
Komaa Concert, lililofanyika jana na kudhaminiwa kwa kiasi kikubwa na Biko.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya Komaa Concert iliyorudiwa leo asubuhi baada ya jana kutopaatikana mshindi katika Tamasha la Komaa lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko Tanzania. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, kushoto akiandika dondoo katika droo ya 27 ya Biko ambapo Viane Kundi wa Iringa, alitangazwa mshindi na kuzoa Sh Milioni 20 za Biko. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Mheshimiwa Paulo Makonda, akizungumza na wadau wa muziki waliofurika katika
Tamasha la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa
Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na
kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala,
aliyepatikana katika droo iliyochezeshwa leo baada ya ndani ya tamasha
kutopokea simu kutokana na wingi wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika
Packers, Kawe. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa EFM Radio, Denis Busurwa
(Sebo). Picha na Mpigapicha Wetu.
Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Dogo Aslay, pichani
akiwachezesha mashabiki wake waliofurika katika Tamasha la Komaa Concert
lililoandaliwa na EFM Radio kwa udhamini mkubwa wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue
Nguvu ya Buku'. Katika Tamasha hilo lililokwenda na kumpata mshindi wa Sh
Milioni limempata Ally Issa Kumburu wa Mwananyamala, aliyepatikana katika droo
iliyochezeshwa jana baada ya ndani ya tamasha kutopokea simu kutokana na wingi
wa watu na kelele za uwanjani Tanganyika Packers, Kawe.
Droo zote mbili zilichezeshwa leo jijini Dar es Salaam kwa
kuendeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki, ambapo ni matokeo ya kutopatikana kwa
mshindi wa tamasha la Komaa Concert, lililofanyika juzi katika Viwanja vya
Tanganyika Packers, Kawe, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika droo hiyo ya 27, Meneja Masoko wa Biko,
Goodhope Heaven, alisema kupatikana kwa washindi hao ni sehemu ya kuendelea
kugawa fedha kwa kwa wote wanaoshinda katika mikoa mbalimbali ya Tanzania,
akiwamo Kumburu wa Komaa Concert, mkazi wa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam
na Viane aliyejinyakulia Sh Milioni 20 akitokea mkoani Iringa.
Alisema Viane amekuwa mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 27,
ambapo anakuwa mmoja kati ya washindi wengi wanaojichotea zawadi nono ya Sh
Milioni 20 kutoka Biko kwa droo ya Jumapili na Jumatano, pamoja na zawadi za
papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh
Milioni moja zinazolipwa moja kwa moja kwenye simu za washiriki wao, huku
akiwataka Watanzania wacheze mara nyingi zaidi ili wajiwekee nafasi nzuri za
kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja Milioni 20 kwa droo ya Jumatano na
Jumapili.
“Jinsi ya kushinda Biko ni rahisi kwa sababu mshiriki
anapaswa kufanya muamala kwenye simu yake kama vile Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel
Money ambapo ataweka Sh 1,000 na kuendelea, huku namba yetu ya Kampuni ni
505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania
kuendelea kucheza Biko ili waibuke na ushindi.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Emmanuel Ndaki, alisema washindi wote wawili wamepatikana kwa kupigiwa simu,
huku akisema kuwa droo ya Tamasha la Komaa Concert imerudiwa ili kujenga
uhalisia, baada ya washindi wote wa jana kutopokea simu.
“Bodi yetu ipo makini kufuatilia michezo hii ya kubahatisha,
hivyo tunawapongeza washindi wote wawili wa Komaa Concert ambaye ni Kumburu wa
Mwananyamala pamoja na binti wa Iringa, anayejulikana kama Viane ambaye naye
ameingia kwenye orodha ya washindi wa mamilioni ya Biko,” Alisema.
Kwa kutangazwa washindi wa Biko, Watanzania hao wenye bahati
wanatarajiwa kukabidhiwa fedha zao mapema wiki ijayo, ikiwa ni mwelekeo wa Biko kutoa
mamilioni ya fedha kwa washindi wao, huku kwa mwezi Mei na Juni pekee ikitoa
zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi mbalimbali wa bahati nasibu yao.
No comments:
Post a Comment