Na Mwandishi Wetu, Mwanza
DROO maalum ya kuwania Sh Milioni 10, iliyoandaliwa na
waandaaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, imeenda kwa kijana mwenye miaka 25,
Said Juma, mkazi wa Mwanza, ikitolewa katika tamasha la burudani la Komaa
Concert la EFM Radio, lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa
jana.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kushoto mwenye kipaza sauti,
akimtangaza Said Juma kulia, aliyefanikiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni
10 za Biko zilizotolewa maalum kwa ajili ya Tamasha la Komaa Concert
lililoandaliwa na EFM Radio Jumamosi iliyopita na kufanyika katika
Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Shabiki wa muziki wa kizazi kipya jijini Mwanza ambaye jina lake halikupatikana mara moja akifuatilia onyesho la Komaa Concert lililoandaliwa na EFM Radio na kudhaminiwa na Bahati Nasibu ya Biko, ambapo pia alitafutwa mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko na Said Juma mkazi wa jijini Mwanza kuibuka kwenye droo hiyo maalum.
Katika tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa jijini Mwanza na
Dar es Salaam, walipata nafasi ya kutoa burudani kwa mashabiki wao, huku
likinogeshwa na Milioni 10 za Biko maalum kwa wakazi wa Mwanza pekee.
Akizungumza katika droo hiyo ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba,
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema mshindi huyo alipatikana kwa
kupigiwa simu kama wanavyopatikana wengine waliowahi kuvuna mamilioni kutoka
kwenye bahati nasibu yao inayochezeshwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa
kupitia mitandao ya simu za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa.
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa jijini
Mwanza, wakiwa katika shangwe kubwa huku mmoja wao akiwa amevaa tshirt
ya Biko wadhamini wa tamasha la burudani la Komaa Concert lililoandaliwa
na EFM Radio kwa udhamini wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko,
ambapo pia ilimtangazaa mshindi wake maalum kwa ajili ya tamasha hilo
ambaye ni Said Juma wa jijini Mwanza aliyezoa Sh Milioni 10 za Biko
Tamasha hilo lilifanyika jana Jumamosi na kufanyika katika Uwanja
wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Alisema kuwa watu waliocheza kwa kufanya miamala kwenye simu
zao kuanzia Sh 1000 na kuendelea walichezeshwa kwenye droo moja iliyompa
ushindi Juma, huku wakicheza kwa kutumia namba ya kampuni ya 505050 na ile ya
kumbukumbu ya 2456.
“Biko limekolea na kuchanja mbuga baada ya leo kumpata kijana
maalum katika droo maalum ya Sh Milioni 10 tuliyoandaa kwa ajili ya tamasha
hili la burudani lililoandaliwa na EFM, ambalo pamoja na mambo mengine,
tuliamua tujumuike na Watanzania wote, hususan wa jijini Mwanza kwa ajili ya
kufurahia pamoja,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko
kwa ajili ya kuwania zawadi za kawaida za papo kwa hapo pamoja na droo kubwa ya
Jumatano na Jumapili ya Milioni 20.
Naye mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku
Salehe, alisema droo hiyo ya Sh Milioni 10 imechezeshwa kwa kufuata sheria,
kanuni na taratibu za michezo ya kubahatisha, huku akiwataka Watanzania
waendelee kutumia fursa ya kucheza Biko.
“Tangu kuanza kwa bahati nasibu ya Biko, Bodi yetu imekuwa
ikifanya kazi kwa karibu na wachezeshaji hawa ili kuhakikisha kwamba kila kitu
kinakwenda vizuri, hivyo tunaendelea kusisitiza kwamba Biko ni mchezo salama na
halali kwa Watanzania wote,” Alisema.
Mbali na kutoa droo hiyo maalum ya Sh Milioni 10, droo
nyingine za kuwania zawadi mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000, 1,000,000 zinazolipwa kwa njia ya
simu za washiriki, pamoja na droo ya Jumatano na Jumapili, huku mwezi Mei na
Juni pekee Biko wakitoa zaidi ya Sh Bilioni moja iliyokwenda kwa washindi wao.
.
No comments:
Post a Comment