Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa droo ya 20 ya Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu
ya Buku’ iliyofanyika Jumatano iliyopita, Philipo Lubeleje, amesema kwamba
donge nono alilokabidhiwa na Biko limeondoa changamoto zake za kimaisha,
kutokana na ugumu wa maisha anaokutana nao kwenye majukumu yake ya kila siku.
Mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Philipo Lubeleje, akiwa kwenye furaha baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 20 zakw kutoka wa waendeshaji wa bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yalifanyika jana katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam.
Lubeleje anayejishughulisha na ujenzi wa nyumba jijini Dar es
Salaam, alikabidhiwa fedha zake jana katika benki ya NMB jijini hapa, huku akisema
amekuwa akiishi maisha magumu, hivyo anazitumia fedha zake vizuri ili akuze
uchumi wake.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Lubeleje ambaye ni
mkazi wa Gongolamboto, jijini Dar es Salaam, alisema amepokea ushindi wake kwa
shangwe sambamba na kumshukuru Mungu kwa kumuona, akiamini kuwa amefanya hivyo
baada ya kubaini kiu yake ya kupata maendeleo ya kiuchumi.
Mshindi wa Sh Milioni 20 ambaye ni mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, Philipo Lubeleje katikati mwenye fulana ya pundamilia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage wa pili kutoka kulia, wakiwa kwenye tukio la kumkabidhi Sh Milioni 20 mshindi huyo wa droo ya 20. Wengine ni ndugu zake pamoja na afisa wa NMB, jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana.
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, kulia akimkabidhi Sh Milioni 20 mshindi wa droo ya 20 ya bahati nasibu ya Biko, Philipo Lubeleje katikati. Mwingine pichani ni Afisa wa NMB jijini Dar es Salaam.
Alisema hata kuamua kucheza bahati nasibu ya Biko kulitokana
na kutafuta fursa za kupata mwangaza wa kiuchumi, akisema kuwa shughuli za
ujenzi wa nyumba zina changamoto nyingi na uhaba wa kazi mara kwa mara.
“Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii ya Sh Milioni 20
kwa kupitia Biko, hivyo naomba Watanzania wenzangu nao wacheze kwa sababu nao
wanaweza kushinda kama mimi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo Pesa,
M-Pesa na Airtel Money, ambapo kama inavyotakiwa, namba ya kampuni ni 505050 na
kumbukumbu ni 2456.
“Huu ni wakati wangu sasa wa kusonga mbele kwa kuanzisha
biashara ambazo zitanipunguzia makali na hatimae kupiga hatua kiuchumi kwa
sababu bahati kama hii inaweza isijirudie katika maisha yangu na kiasi
nilichokabidhiwa si kidogo,” Alisema Lubeleje.
Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage,
alisema mbali na ushindi wa Sh Milioni 20 unaotoka katika droo ya Jumatano na
Jumapili, pia watu wanaweza kuvuna zawadi za papo kwa hapo ambapo ni fedha
taslimu zinazoanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh
Milioni Moja.
“Biko imekuja kwenu Watanzania kuwapatia fedha nyingi ambazo
kila mtu anaweza kushinda, hivyo kinachotakiwa ni kucheza mara nyingi, huku
tukianzia kucheza kwa SH 1,000 tu, ambapo kiasi hicho cha pesa kitatoa nafasi
mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo ya kuwania Sh
Milioni 20 Jumatano na Jumapili,” Alisema Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.
Tayari Biko waendeshaji hao wa bahati nasibu ya aina yake
wameshatoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa mwezi Mei na Juni, huku fedha za
ushindi zikilipwa haraka kwa njia ya benki ya NMB kwa wale wanaoshinda ushindi
mkubwa bila kusahau wanaolipwa kwenye simu zao dakika chache baada ya kupokea
ujumbe unaomtaarifu kushinda kwake zawadi za papo kwa hapo.
No comments:
Post a Comment