Na Mwandishi Wetu, Mtwara
MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, jana
amekabidhiwa fedha zake alizoshinda kutoka kwa waendeshaji wa Bahati Nasibu ya
Biko, jumla ya Sh Milioni 20.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana mkoani Mtwara katika benki
ya NMB, ambapo Lukinga aliishukuru Biko na kusema kuwa fedha hizo atazitumia
vizuri kuhakikisha zinakuza uchumi wake.
“Nashukuru kwa kukabidhiwa fedha hizi ambazo kwa hakika
nitazitumia vizuri kama sehemu ya kupiga hatua kiuchumi kama dhamira ya Biko
kuanzisha bahati nasibu yao.
Meneja Masoko wa Bahati Nasibu ya
Biko Tanzania, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia, akimkabidhi jumla
ya Sh Milioni 20 mshindi wao wa mjini Mtwara, Ally Hassan Lukinga
aliyeshinda katika droo ya 24 Jumapili. Kulia ni Mratibu wa Matukio na
Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles.
“Awali sikuamini kama naweza kushinda donge nono la Sh
Milioni 20, hivyo ni wakati huu Watanzania wote kuamini kwamba Biko ni mchezo
wa kubahatisha wa watu wote, maana kama hata mimi wa Mtwara nashinda, ndio
kusema yoyote anaweza kushinda,” Alisema.
Ally Hassan Lukinga kulia akifurahia fedha zake alizokabidhiwa na Biko mkoani Mtwara.
Naye Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko Tanzania, Hassan
Melles, alimpongeza Lukinga kwa kukabidhiwa fedha zake, huku akiwataka
Watanzania wote kuchangamkia fursa ya Biko ili washinde zawadi za papo kwa hapo
kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja
zinazotoka kila wakati, sambamba na droo kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka
Jumatano na Jumapili.
“Jumapili hii amepata Lukinga ambapo leo tumemkabidhi fedha
zake, hivyo wote mnaweza kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo
Pesa, M-Pesa na Airtel Money, ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ya
kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea kikiwa Sh 1,000 na kuendelea,”
Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba
Biko inaendelea kutoa zawadi mbalimbali zikiwapo za papo kwa hapo na zile za
Milioni 20, hivyo yoyote atakayeshinda katika Mkoa wa Tanzania atafikishiwa
fedha zake haraka iwezekanavyo ili azitumie kwa ajili ya maendeleo yake.
“Kumpatia fedha zake Lukinga wa mjini Mtwara ni nafasi ya
kumsubiri mwingine aibuke na mamilioni ya Biko ili naye apate chake, maana Biko
ipo kwa ajili ya Watanzania wote, hivyo dawa ya ushindi ni kucheza mara nyingi
zaidi wakati wowote na mahala popote kwenye mikoa yote ya Tanzania,” Alisema.
Baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Mtwara, mshindi
mwingine wa Sh Milioni 20 anatarajiwa kupatikana Jumatano ama (Jumatamu) kama
wanavyoita, ikiwa tayari Biko wameshakabidhi zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi
ya Mei na Juni pekee.
No comments:
Post a Comment