Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MFANYAKAZI wa Tanesco mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga, ameibuka
na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko katika droo
ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam.
Lukinga fundi wa Tanesco alitangazwa mshindi na Balozi wa
Biko, Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Abdallah Hemed.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed
kushoto akiandika maelezo ya mshindi wa donge nono la Sh Milioni 20
alilopata mfanyakazi wa TANESCO Mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga mara
baada ya kupatikana kwenye droo ya 25 iliyochezeshwa leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja. Picha na Mpigapicha
Wetu.Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja, kulia akionyesha pozi nzito baada ya kupatikana mshindi wa Sh Milioni 20 kutoka mkoani Mtwara, Ally Hassan Lukinga aliyetengazwa katika droo ya 25 iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.
Akizungumza katika droo hiyo, Mratibu wa Matukio na
Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema ni mara ya kwanza kumpata mshindi
wa droo kubwa ya Sh Milioni kutoka Mkoa wa Mtwara.
Alisema kupatikana kwa mshindi huyo kunaongeza wigo wa
washindi wa Biko kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wanaoshinda droo kubwa
pamoja na wanaoibuka na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000,
20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.
“Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mchezo wetu wa
kubahatisha tumempata mshindi kutoka Mtwara, ambaye ni fundi wa Tanesco, huku
tukiamini kuwa kila mtu anaweza kuibuka na ushindi kutoka Biko endapo atacheza
mara nyingi zaidi kwa kupitia mitandao ya simu.
“Biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya
miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya
kampuni ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456, huku gharama za uchezaji
zikianzia Sh 1,000 na kuendelea, ambapo shilingi 1000 inatoa nafasi mbili ambazo
ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni
20 inayotolewa kila Jumatano na Jumapili,” Alisema Melles.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Abdallah Hemed, alimpongeza Lukinga kwa kuibuka na ushindi huo mnono, huku
akisema Biko ni mchezo unaochezwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zote
zilizowekwa katika tasnia ya michezo ya kubahatisha.
“Bodi yetu inakuwa karibu kuhakikisha kwamba washindi wetu
wanapatikana kihalali, ambapo safari hii mkazi wa Mtwara, Lukinga ameibuka
kidedea kwa kupata donge nono la Biko la Sh Milioni 20,” Alisema.
Naye Lukinga akizungumza kwa simu wakati anahojiana na Kajala,
Balozi wa Biko, alisema haamini kabisa kama ameshinda zawadi nono ya Biko,
akipigiwa simu kuambiwa hilo dakika chache baada ya namba yake kushinda.
“Nashukuru sana kwa kushinda zawadi hiyo nono kutoka Biko,
maana siku ushindi huo umeniaminisha kuwa watu wanashinda kihalali, hivyo huu
ni wakati wangu kufurahia maana hata jana nilicheza Biko,” Alisema.
Kwa kushinda donge nono la Biko, Lukinga anatarajia kupokea
fedha zake haraka wiki hii, ikiwa ni mwendelezo wa bahati nasibu hiyo kutoa
zawadi za fedha za papo kwa hapo pamoja na donge nono la Sh Milioni 20
zinazotolewa Jumatano na Jumapili, huku mwezi Mei na Juni pekee Biko wakitoa
zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wao.
No comments:
Post a Comment