Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WITO umetolewa kwa washindi wa
bahati nasibu ya Biko wanaoendelea kupatikana kila siku wafanye vitu vya
maendeleo mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao za fedha kutoka kwenye bahati
nasibu hiyo ya aina yake.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, kulia akimkabidhi
kiasi cha Sh Milioni 20 mshindi wao Fredy Nyari wa Kigamboni aliyeibuka na
ushindi mnono wa Sh Milioni 20 katika droo ya 23 juzi. Kushoto ni Afisa wa NMB.
Hayo yamesemwa na Meneja Masoko wa
Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alipokuwa anamkabidhi jumla ya Sh Milioni 20
mshindi wa Jumadili (Jumapili), Fredy Nyari, akiwa ni mshindi wa droo ya 23 ya
Biko.
Akizungumzia hatua ya makabidhiano
ya fedha hizo, Heaven, alisema kwamba ikiwa siku zote mtu anakosa mtaji wa
kuanzisha au kuendeleza biashara zake, kupata Milioni 20 kwa mara moja si jambo
la mzaha.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko droo ya 23, Fredy Nyari,
akiwa na uso wa furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB,
jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akiwa na mshindi
wao wa Sh Milioni 20 Fredy Nyari baada ya kumkabidhi fedha zake katika benki ya
NMB, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Alisema ni wakati wao sasa washindi
wote wa Biko wale wanaopata zawadi nono ya Sh Milioni 20 inayotoka kila
Jumatano na Jumapili pamoja na zawadi za papo kwa hapo zinazoanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja wanakuza uchumi
wao.
“Kwa kuanzia Sh 1,000 tu mtu
anaweza kushinda 5,000 hadi Milioni 20 kwa droo zetu kubwa, ambapo ni rai yetu
kwa washindi wote kuwataka maisha yao yabadilike kwa kutumia vyema fedha zao
baada ya kucheza Biko, mchezo unaochezwa kwa kufanya miamala kwenye simu za
TIGO Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba yetu ya Kampuni ni 505050 na ile
ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Heaven.
Naye Nyari, mshindi huyo wa droo ya
23 aliyotangazwa juzi jijini Dar es Salaam, alisema ni jambo la kumshukuru
Mungu kwa hatua yake ya kuibuka na ushindi wa Sh Milioni 20 uliokuja kuyabadili
maisha yake baada ya kukabidhiwa jana katika Tawi la Benki ya NMB, jijini Dar
es Salaam.
“Wakati napigiwa simu ya ushindi na
balozi wa Biko, Kajala Masanja, hakika nilikuwa siamini, ukizingatia kuwa
wanaocheza Biko ni wengi na kila mtu anataka yeye awe mshindi wa Jumatano au
Jumapili, hivyo kwangu mamilioni haya niliyokabidhiwa leo yamekuja
kunibadilisha kwa hatua moja kwenda nyingine.
“Nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha kwamba napiga hatua kubwa, ili pamoja na mambo mengine, niweze
kutimiza ndoto zangu na kuwaaminisha waendeshaji wa mchezo wa Biko kuwa fedha
zao zinabadilisha maisha yangu kiuchumi,” Alisema.
Moja ya sifa kubwa ya bahati nasibu
ya Biko ni kitendo chake cha kuwakabidhi washindi wao fedha zao wanazoshinda
siku moja tu baada ya kutangazwa washindi jambo linaloongeza chachu ya kupiga
hatua kimaendeleo, huku kwa kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, wakiweza
kuwapa washindi wao zaidi ya Sh Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu
yao.
No comments:
Post a Comment