Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MBUNGE wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, leo
mjini hapa, amemkabidhi mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko,
Elizabeth Damian, aliyetangazwa mshindi katika droo ya 22 ya bahati nasibu hiyo
inayojulikana pia kama ‘Ijue Nguvu ya Buku’ iliyofanyika juzi Jumatano, jijini
Dar es Salaam.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Mheshimiwa Abdulaziz Abood, kushoto akimkabidhi hundi ya Sh Milioni 20 mshindi wa Biko Morogoro saa chache kabla ya kukabidhiwa fedha taslimu katika benki ya NMB, mjini hapa jana. Anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wa pili kutoka kulia.Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood wa tatu kutoka kulia akimkabidhi jumla ya Sh Milioni 20 mshindi wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian wa pili kutoka kushoto. Wa kwanza kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven wakati wanamkabidhi mshindi huyo katika Tawi la benki ya NMB Morogoro jana.
Akizungumza katika makabidhiano ya Sh Milioni 20 mjini Morogoro jana, Mbunge Abdulaziz,
alisema bahati nasibu ni mchezo unaoweza kutoa fursa nzuri kiuchumi, huku
akimtaka mshindi huyo azitumie vizuri pesa zake ili ziweze kumnufaisha
kiuchumi.
Alisema kwamba jinsi mchezo wa Biko unavyochezeshwa ni sehemu
muafaka ya kuhakikisha kwamba kila mtu anatumia vyema fursa ya kupiga hatua
kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, hivyo wananchi wake wa Morogoro na
Watanzania wote kwa ujumla waendelee kucheza ili wavune fedha za ushindi.
Mshindi wa Shilingi Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya
Buku', Elizabeth Damian baada ya kukabidhiwa jana mjini Morogoro.
Duh! Siamini kama fedha zote hizi zangu! Ndivyo anavyoonekana kusema, mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko aliyepatikana mkoani Morogoro ambapo jana alikabidhiwa mzigo wote.
“Wakati nawapongeza Biko kwa kubuni michezo hii inayotoa
mamilioni kwenu washindi, lakini pia nakupongeza wewe mwananchi wangu wa
Morogoro kwa kuwa kati ya wachezaji wenye bahati kubwa kiasi cha leo
kukabidhiwa Sh Milioni 20,” Alisema.
Akizungumzia ushindi wake, Elizabeth aliyekabidhiwa fedha
zake katika benki ya NMB, mjini Morogoro, alisema hakuamini kama angeweza
kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 kutoka Biko, jambo linalomfanya furaha
yake isielezeke.
“Kwa kweli siamini kama leo nimekabidhiwa fedha zangu kiasi
cha Sh Milioni 20 nilizopata kutoka kwa Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania
wenzangu kucheza kwa wingi bahati nasibu hii maana ushindi upo nje nje na fedha
zangu nitazitumia vizuri kwa mambo mengi kama vile biashara na ujenzi wa nyumba,”
Alisema.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kuacha
kucheza Biko ni kukubali kukosa fursa za kiuchumi ambazo kila mtu anaweza
kuzipata kwa kucheza mara nyingi bahati nasibu yao inayochezwa kwa njia ya
ujumbe mfupi wa maandishi wa Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel kwa kufanya miamala
kwenye simu zao kuanzia Sh 1000 na kuendelea.
“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu tiketi moja ya Sh 1000
inapofanywa kwa njia ya muamala kwenye simu husika, itampatia nafasi mbili za
ushindi wa papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000,
500,000 na Sh Milioni moja, pamoja na donge nono la Sh Milioni 20
zinazopatikana kila Jumatano na Jumapili, huku namba ya kampuni yetu ikiwa ni
505050 na kumbukumbu namba ni 2456.
“Kila mtu anaweza kushinda zawadi nono kutoka Biko, hivyo
unachotakiwa kufanya ni kucheza mara nyingi zaidi kama njia ya kujiwekea
mazingira mazuri ya ushindi mnono kutoka kwenye bahati nasibu yetu ya Biko,”
Alisema Heaven.
Tangu kuanza kwa bahati nasibu ya Biko nchini Tanzania ikiwa
ni miezi miwili tu, tayari imeshatoa zaidi ya Sh Bilioni moja kwa washindi wake
katika kipindi cha mwezi Mei na Juni pekee, ikiwa ni ishara kuwa Watanzania
wengi wamekuwa wakiitumia fursa ya kuvuna mamilioni kutoka Biko.
No comments:
Post a Comment