FUNDI ujenzi Phillip Luberege mwenye maskani yake
Gongolamboto jijini Dar es Salaam, ametangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya
Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, akipatikana katika droo ya 20 ya kuwania Sh Milioni
20.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akionyesha namba ya mshindi wa Sh Milioni 20 aliyopata mkazi wa Gongolamboto, Phillip Luberege. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Kajala Masanja kulia akiwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Luberege ametangazwa mshindi leo jijini Dar es Salaam katika
droo ya 20 iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, akishirikiana na
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope
Heaven, alisema mshindi huyo amepatikana baada ya kupatikana kwa washindi wa
mikoani kiasi cha kuashiria kwamba kumekuwa na mwamko mkubwa kutoka kona zote
za Tanzania kuchangamkia mchezo wao kwa watu kuchangamkia fursa ya ushindi wa
papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh
Milioni moja.
Alisema kwamba mchezo wao wa Biko ni rahisi kucheza pamoja na
kushinda, kwa sababu unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa
kufanya miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba
ya kampuni yao ni 505050 na kumbukumbu yao ni 2456, huku kiasi cha kuanzia
kucheza kikiwa ni Sh 1000 na kuendelea.
“Sh 1000 ya kucheza Biko inampa mshiriki wetu nafasi mbili ya
ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh
Milioni 20 ambapo hufanyika Jumatano na Jumapili, huku mpaka sasa Biko ikitoa
zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na Juni pekee,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Chiku Salehe alisema kwamba maofisa wa Bodi yao wamekuwa wakihudhuria droo zote
za Biko, huku wakisema kuwa mchezo huo umekuwa ukichezeshwa kwa kufuata sheria,
kanuni na taratibu zote.
“Biko ni mchezo unaofuata sheria zote, hivyo ni salama ambapo
kwa wiki hii amepatikana mshindi wa Gongolamboto, baada ya kuchezeshwa droo ya
kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 ya Jumatano,” Alisema.
Kwa Mwezi Mei na Juni pekee, waendeshaji hao wa mchezo wa
kubahaisha wa Biko wametoa zaidi ya Sh Milioni Bilioni moja tangu kuanzishwa kwa
mchezo huo unaotikisa katika viunga mbalimbali vya Tanzania.
No comments:
Post a Comment