Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZAWADI nono ya Sh Milioni 20 zinazotolewa na Bahati Nasibu ya
Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, zimekimbiza homa ya mshindi wa droo ya 24 ya Biko,
iliyotangazwa leo jijini Dar es Salaam, huku akiipata mkazi wa Chanika, jijini
Dar es Salaam, Enos Marianus.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza kwa simu na mshindi wa droo ya 24
ya Biko , Enos Marianus, aliyejizolea jumla ya Sh Milioni 20
atakazokabidhiwa haraka wiki hii. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed, akiandika dondoo za
mshindi huyo wakati anazungumza kwa njia ya simu mara baada ya namba
yake kuibuka kidedea katika droo hiyo ya 24. Picha na Mpigapicha Wetu.
Akizungumza kwa njia ya simu wakati anapewa taarifa za
ushindi wake na Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Marianus alisema kwamba
amekuwa mchezaji mzuri wa Biko, huku habari za ushindi wake zikiikimbiza homa
iliyokuwa inamsumbua kwa wiki moja sasa.
Marianus alisema kwamba ushindi wa Sh Milioni 20
aliyotangazwa na Biko utakuwa muafaka kwake kutokana na kujihusisha na biashara
ndogo ndogo kwa ajili ya kusukuma mbele gudurumu la maisha yake.
“Nashukuru sana kwa kunitangaza mimi kuwa ni mshindi wa droo
ya 24 ya Biko, hivyo hapa hata homa inayonisumbua imeondoka na nimepona kabisa
kwa sababu ya habari zenu nzuri, nikiamini kwamba nikipata fedha hizo nitapiga
hatua kubwa kiuchumi hususan katika biashara zangu,” Alisema Marianus.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba
droo ya Jumatano imekwenda kwa mfanyabiashara mdogo wa Chanika, huku akiwataka
wengine waendelee kucheza kwa ajili ya kuvuna donge nono la Sh Milioni 20 kwa
Jumatano na Jumapili, pamoja na zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000,
10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja.
“Biko ni mchezo rahisi kushinda na unaweza kubadilisha maisha
ya Watanzania, hivyo endeleeni kucheza kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo
Pesa, M-Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku kiasi cha
fedha cha Sh 1000 kikitoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na
kuingia kwenye droo kubwa za Sh Milioni 20 za Jumatano na Jumapili, namba ya
kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Abdallah Hemed, alisema mchezo
wa Biko unachezeshwa kwa kufuata sheria zote za michezo ya kubahatisha, huku
akiwataka Watanzania kuuamini na kutumia fursa za ushindi kwa ajili ya maisha
yao.
Biko ni mchezo wa kubahatisha unaotikisa katika viunga
mbalimbali vya Tanzania, huku mwezi Mei na Juni pekee ukitoa zaidi ya Sh
Bilioni moja kwa washindi wake walioshinda zawadi mbalimbali kutoka kwenye
bahati nasibu hiyo, huku mshindi wa droo ya 24 akitarajiwa kukabidhiwa fedha
zake haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment