Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya 22 ya waendeshaji wa mchezo wa kubahatisha wa Biko ‘Ijue
Nguvu ya Buku, imefanyika leo jijini Dar es Salaam, huku mkazi wa Morogoro,
Elizabeth Damian akifanikiwa kutangazwa mshindi wa Sh Milioni 20 zinazotolewa
na bahati nasibu hiyo.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Biko, Yassin Lohai akipiga picha ya shangwe
baada ya kukabidhiwa fedha zake katika tawi la Madaraka la NMB jijini
Tanga leo mchana. Lohai alikabidhiwa na Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven
hayupo pichani.
Mwanadada huyo kutoka mkoani Morogoro, alitangazwa mshindi
katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja kwa
kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari
Maggid.
Akizungumza katika droo hiyo, Kajala aliwataka Watanzania
kuendelea kucheza Biko ili wajiweke katika nafasi nzuri ya kuvuna mamilioni
yanayotolewa na Biko tangu kuanzishwa kwake, huku hadi sasa kwa miezi miwili ya
Mei na Juni, zaidi ya Sh Bilioni moja zikienda kwa washindi.
Alisema fursa inayotolewa na Biko ni nzuri kwa uchumi wa
Watanzania kwa kuhakikisha kwamba wanacheza Biko mara nyingi zaidi ili
wajiwekee mazingira mazuri ya kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh
5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, sambamba
dau nono la Sh Milioni 20 linalotoka kila Jumatano na Jumapili, kianzio cha
kucheza kikiwa Sh 1000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ya Biko ikiwa ni
505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven kulia akimkabidhi Sh Milioni 20
mshindi wa Tanga, Yassin Lohai baada ya kushinda donge nono la Biko
Jumapili iliyopita. Kushoto ni Afisa wa NMB, Tawi la Madaraka, jijini
Tanga, akishuhudia makabidhiano hayo kwa mshindi wa Biko mkoani Tanga.
Balozi wa Biko Kajala Masanja, kulia akisalimiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid, katika droo ya kumtafuta mshindi wa Milioni 20 wa droo ya 22, ambapo Elizabeth Damian alitangazwa mshindi leo asubuhi.
“Tangu Biko ianze kuchezeshwa Tanzania imekuwa ikitoa nafasi
kubwa ya Watanzania kuvuna mamilioni, hivyo nawashauri Watanzania wenzangu
kujitokeza kwa wingi kucheza Biko ili nao waweze kuvuna fedha zinazotolewa Biko
kwa zawadi za papo kwa hapo pamoja na zile wiki ambazo ndio kubwa zaidi,
nikiamini kuwa endapo mtu anafanikiwa kuzipata, naamini atapiga hatua kubwa
kiuchumi,” Alisema Kajala.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Bakari Maggid, alisema Biko ni mchezo rahisi na halali unaofuata sheria zote,
hivyo wanaamini Watanzania wataendelea kutumia fursa za kucheza mchezo huo wa
kubahatisha wa Biko.
“Bodi yetu imekuwa ikihudhuria droo zote za Biko na leo
amepatikana mkazi wa Morogoro anayejulikana kwa jina la Elizabeth Damian, hivyo
tunampongeza kwa ushindi wake pamoja na kuwahakikishia usalama mkubwa juu ya
mchezo huu,” Alisema.
Katika hatua nyingine, mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya
21 kutoka mkoani Tanga, Yassin Lohai, leo amekabidhiwa fedha zake, huku
akiwashukuru Biko na kuahidi kuwa atazitumia vizuri fedha zake katika hali ya
kuziingiza katika harakati za kumletea maendeleo makubwa.
“Nashukuru Mungu kwa kukabidhiwa fedha zangu Sh Milioni 20
kutoka Biko, hivyo nawakumbusha Watanzania wenzangu kuwa mchezo huu ni kweli
washindi wanapewa zawadi zao haraka, jambo linaloweza kutusaidia kutukwamua
kiuchumi,” Alisema Lohai na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alisema kuwa
Biko unazidi kuchanja mbuga kwasababu washindi wengi wa papo kwa hapo wamekuwa
wakipatikana sambamba na wale wanaoibuka na mamilioni 20 wanaoshinda na
kukabidhiwa fedha zao haraka kwa ajili ya kuwapatia mwangaza wa kiuchumi.
Kwa miezi miwili ya Mei na Juni, washindi wa Biko wameshinda
na kukabidhiwa fedha zao zaidi ya Sh Bilioni moja, jambo linalotafsiriwa kuwa
ni sehemu ya kuwakwamua Watanzania wanaoitumia fursa ya uwapo wa mchezo wa
kubahatisha wa Biko unaochezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi kwa kufanyaa
miamala kwenye simu za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money.
No comments:
Post a Comment