Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Kigamboni, jijini Dar es Salaam leo amefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20 baada ya kutangazwa
mshindi katika kinyang’anyiro cha droo ya 23 ya Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue
Nguvu ya Buku’, inayoendelea kutesa hapa nchini.
Droo iliyompa ushindi mnono mkazi huyo wa Kigamboni maarufu
kama ‘Jumadili’, imechezeshwa jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko Kajala
Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Bakari Maggid.
Mwakilishyi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari
Maggid kushoto akiandika dondoo muhimu katika droo ya 23 ya Bahati
Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku' leo jijini Dar es Salaam, ambapo
mkazi wa Temeke, Fredy Nyari alifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh
Milioni 20 kutoka Biko. Kulia ni Balozi wa Biko Tanzania, Kajala
Masanja.Picha na Mpigapicha Wetu.
Harakati za kumtafuta mshindi wa droo ya 23 Fredy Nyari wa Kigamboni jijini Dar es Salaam, zilipofikia ukomo kwa Balozi wa Biko, Kajala Masanja kutoa neno kwa wadau na Watanzania kwa ujumla juu ya bahati nasibu ya Biko.
Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.
Akizungumza katika droo hiyo ya aina yake, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kumpata mshindi wao wa Kigamboni ni sehemu ya kuhakikisha kuwa washindi wao wanaendelea kuzoa mamilioni kutoka kwao baada ya kucheza Biko.
Alisema kila anayecheza Biko anasehemu kubwa ya kuibuka na
ushindi wa zawadi za papo kwa hapo pamoja kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000,
50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja bila kusahau donge nono la Sh
Milioni 20 linalotoka katika droo kubwa za Jumatano na Jumapili.
“Kucheza Biko ni rahisi kwa sababu mchezo wetu wa kubahatisha
unachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kupitia miamala ya kifedha
kuanzia Sh 1,000 na kuendelea ambapo namba zetu za kampuni ni 505050 na ile ya
kumbukumbu ni 2456.
“Ili mtu aweze kushinda anapaswa kucheza mara nyingi zaidi
kwa kuanzia Sh 1000 na kuendelea ambapo mbali na ushindi wa papo kwa hapo
unaotoka kila wakati, pia ni fursa nzuri ya droo kubwa ya Sh Milioni 20 ambazo
tunaamini mtu akifanikiwa kuzipata kama alivyopata mshindi wetu wa Kigamboni
bwana Nyari maisha yake yatapiga hatua kubwa,” Alisema.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania,
Bakari Maggid, alimpongeza Nyari wa Kigamboni kwa kuwa mmoja kati ya vijana
wadogo wanaoibuka na mamilioni ya Biko tangu kuanzishwa kwa bahati nasibu
inayotesa nchini inayochezwa kwa njia ya ujumbe wa maandishi.
“Kuwapo kwetu katika droo kuna maana kuwa bahati nasibu hii
ni halali na ina nia njema kwa Watanzania, hivyo tunawajulisha Watanzania wote
juu ya kutumia michezo kama hii ili kuboresha kipato chao endapo mtu atafanikiwa
kushinda zawadi mbalimbali kama wanavyoshinda watu tofauti kutoka kila pembe za
nchi yetu ya Tanzania,” Alisema.
Wiki iliyopita, mshindi wa Morogoro Mjini, Elizabeth Damian
alifanikiwa kukabidhiwa zawadi yake ya Sh Milioni 20 ikiwa ni siku moja baada
ya kutangazwa mshindi katika droo ya 22 ya Biko, huku bahati nasibu hiyo
ikiweza kuwapa washindi zaidi ya Sh Bilioni moja kwa miezi miwili ya Mei na
Juni pekee kama sehemu ya ushindi wa pesa mbalimbali walizoshinda.
.
No comments:
Post a Comment