MECHI namba 163 ya Ligi Kuu ya
Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi
Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.
Kipa wa Simba, Juma Kaseja
Watazamaji 3,145 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho
kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 2,841 na
kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki ilikuwa ya kiingilio
cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh. 720,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi
sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 422,877.41.