Pages

Pages

Thursday, April 25, 2013

Ally Choki aapa kuwanyakua wa kuipaisha zaidi Extra Bongo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Next Level, Ally Choki, amesema kwamba yupo kwenye mikakati ya kuwanyakua na kuwatambulisha waimbaji wasiozidi watatu kwa ajili ya kuimarisha zaidi safu yao.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki
Extra Bongo imezidi kuteka nyoyo za wapenzi wao, huku shoo zao zikipendwa na watu wengi katika kumbi mbalimbali za starehe nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Choki alisema kwamba anaamini kufanikiwa kuwapata waimbaji wao mambo yao yatakuwa mazuri katika hali ya kujiweka sawa kiushindani.

Alisema ingawa kwa sasa bendi yao ipo juu kimuziki, lakini bado wanahitajika wa kuleta ushindani kwa kuhakikisha kuwa waimbaji wenye vipaji na uwezo wa juu wanaingia katika bendi yao.

“Huu ni wakati wa kuhakikisha kuwa Extra Bongo inazidi kuwika katika nyanja za Kitaifa na Kimataifa, hivyo naamini endapo tutafanikiwa kuwanasa waimbaji hao wawili au watatu, kila kitu kitakuwa sawa.

“Sisi ni watu wa kazi si wa kupiga porojo, hivyo jukumu letu kwa sasa ni kuendelea na mazungumzo na hao ambao tumewaomba tuwe nao katika kuimarisha bendi yetu ya Wazee wa Kizigo,” alisema.

Bendi hiyo kwa sasa imesheheni waimbaji wenye uwezo wa kutisha, akiwamo Ramadhan Masanja Banza Stone, Rogati Hega Katapila, Khadija Kimobiteli Athanas na wengineo.

No comments:

Post a Comment