Pages

Pages

Saturday, April 27, 2013

Asha Baraka ampiga mkwara mzito Ally Choki


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKURUGENZI wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka, amempiga mkwara mzito Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki kwa kumueleza kuwa aache kuwafuatilia wanamuziki wake kwa lengo la kuiangusha bendi yake inayotesa hapa nchini.
 Ally Choki
Asha Baraka
Choki amekuwa kwenye mikakati ya kuimarisha safu ya Extra Bongo, huku akiwatolea macho wanamuziki kadhaa kwa ajili kuiweka sawa bendi yake hiyo ya Wazee wa Kizigo.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Asha aliyerejea hivi karibuni akitokea nchini India, alisema kwamba ameambiwa mkakati wa choki kutaka kuibomoa bendi yake hiyo, jambo ambalo analichukulia kwa umakini mkubwa.

alisema Extra Bongo ni bendi yenye wanamuziki wazuri, hivyo hakuna haja tena ya kuhangaika na waimbaji waliokuwa kwingine, hasa kama lengo ni kuiweka sawa bendi yake.

“Kama anataka kumwaga Milioni 10 au zaidi kwa mwanamuziki mmoja aliyekuwa Twanga Pepeta au kwingine, ni wazi hizo fedha awape waimbaji wake ambao kwa hakika wanafanya kazi nzuri.

“Lakini kupita tena kwangu na kuwataka waimbaji wengine si kitendo cha kiungwana, hivyo hili lazima wadau walijuwe kama lengo ni kukuza muziki wa dansi nchini,” alisema.

Kwa mujibu wa Asha Baraka, Choki amepanga kuwachukua waimbaji wake akiwamo Dogo Rama, Salehe Kupaza Mwanatanga na wengineo, kama mkakati wake wa kuingusha Twanga Pepeta.

No comments:

Post a Comment