Pages

Pages

Tuesday, April 30, 2013

Bondia Japhet Kaseba kuzipiga na Mkenya Joseph Magudha Mwezi wa sita

Mwili chuma
                        Taratibu zikiendelea, akiwapo Pendo Njau anayeandika



             Mabondia wakionyeshana ubabe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA mwenye uwezo wa kutisha nchini, Japheti Kaseba, anatarajia kuzipiga na bondia kutoka nchini Kenya, Joseph Magudha mwishoni mwa mwezi wa sita huku kila mmoja ikiwa ni njia yake ya kuonyesha umwamba. 
Mdau wa ngumi nchini, Ibrahim Kamwe, alisema kuwa mchezo huo utatoa picha kamili ya ubabe wa mabondia hao.


Hivyo maandalizi yameanza kuandaa mabondia watakaocheza utangulizi, kwa kuweka mapambano makali likiwemo la kamanda wa makamanda atakaezipiga na Ibrahim Maokola.

Mwanzoni maokola alikuwa amepangwa azipige na bondia toka moro na kamanda kupewa bondia mwingine, lakini kulitokea kupishana kwa maneno kati ya mabondia hao kiasi cha kutaka kupigana kavu.

Mabondia na viongozi waliokuwepo hapo akiwemo ibrahim kamwe walipendekeza ibadilishwe wapinzani na wawili hao wazipige kukata ngebe na majigambo ya ubabe waliyokuwa wakitupiana.

Mpaka sasa mapambano ya utangulizi inategemea kuwa juma seleman atazipiga na issa Omar, Juma fundi atapigana na Moro Best, wakati Yohana Mathayo atazipiga na Joseph Onyango toka Kenya.

No comments:

Post a Comment