Pages

Pages

Saturday, April 27, 2013

MAMBO FULANI MUHIMU

Ukijirahisi, kwenye mapenzi imekula kwako
Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
INASHANGAZA kuona msichana anajirahisi katika suala zima la mapenzi, kwa madai eti anaonyesha uhalisia wake wa upendo kwa mwanaume, anayefanya naye kazi, anayeishi mtaani kwao au amekutana naye sehemu Fulani na kuona anafaa kuwa naye.
Pozi la aina yake la wapenda nao
Ni kweli kuwa yoyote anastahili kupenda au kupendwa mahala anapodhani panafaa, ila kuna miiko yake. Kumbuka, unaposhindwa kuzuia hisia zako, tena mahali pasipokuwa muafaka, ni wazi unahitaji kudhalilika kama sio kudhalilishwa na huyo umpendae.
Zipo kanuni zake. Hata shamba, linahitaji maandalizi, yakiwamo ya kulima au kupapaliwa baada ya kupandwa kwa mazao husika, hivyo inapotokea wewe umekurupuka katika suala la mapenzi, jua itakula kwako.

Kwanini nasema hivyo, wapo wasichana ambao wameshindwa kutambua namna ya kufikisha hisia au ujumbe wa mapenzi kwa wanaume wawatakao na kujikuta wakijiachia ovyo ovyo.
Ndio hapo mtu anapofanya vituko, iwe vya kuonyesha nyeti zake kwa mwanaume ambaye anajua kuwa 
akifanya hivyo yule mtu atajua kuwa anampenda.

Kwa wale wanaoishi mtaa mmoja, mara nyingine hukutana na binti ambaye anajitia kuinama chini na kuonyesha maungo yake wazi. Hata hivyo haitoshi, hufikia kuonyesha titi zao wazi kwa kuvaa nguo ambazo si muafaka kwao.

Kwa mfano, kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kukutana na msichana ambaye bila kujua anachofanya, hufikia kujionyesha ovyo kwa mwanaume kisa anataka awe naye kwenye uhusiano wa kimapenzi.
Kwa bahati mbaya, mtu huyo hajajua thamani halisi ya moyo wake na huyo mtu akifanikiwa kuwa naye, atakuwa na mapenzi ya dhati?

Huu sio mwendo mzuri. Kila mtu anapaswa kujiangalia na kufahamu njia anazopaswa kupita kwa ajili ya mtu wake. Kwa mfano, unapojionyesha bila mpango, hakika kuna uwezekano mkubwa ukaonekana ni kicheche, mwanaumke ambaye ni mwenye tabia za ukahaba.

Hata huyo unayedhani atakupenda, utampa shughuli za kukuchunguza na mwishowe kujiridhisha kuwa si mwanamke wa kutulia naye zaidi ya kukudharau.

Haya hutokea sana. Na yanapotokea katika jamii, wapo wanaochekwa ujinga, hasa wale wanaodhani kila mtu anastahili kuonyeshwa upendo kwa namna moja ama nyingine.

Ndio maana nasema, kuna njia nzuri za kiungwana za kufikisha ujumbe kwa mtu unayetaka kuwa pamoja katika mapenzi na sio njia za kujiachia ovyo, kujichekesha bila mpango.

Huo ndio mpango na ambao hakika ukiufanya watu hawawezi kukuona ni Malaya unayejiuza kwa watu. Tena katika mitandao ya kijamii ndio kabisa. Mtu anaweza kushangaza anaposema anampenda mtu fulani, ambaye hajawahi kukutana naye hata siku moja, tena akaanza kujipendekeza, kujirahisi kuonyesha dalili za mapenzi.

Hayo ya mitandao nitayajadili siku nyingine nikiwa na afya na nafasi, ila ikifikie wakati jamii, hasa watoto wa kike kutambua namna nzuri za kulinda heshima zao kwenye suala zima la mapenzi.

Wakifanya hivyo, kila mtu atakuwa na sababu za kutembea kifua mbele, akiheshimika baada ya kujiheshimu kwa namna moja ama nyingine. Mengi yamekuwa yakiwatesa na kuwasumbua watu.

Tena huko kutaka kufikisha ujumbe wako kwa mtu, unaweza kuufikisha kistaarabu, kutetea msimamo wako, kuwa mkali na wapiti njia, kuhakikisha kuwa kila mtu anakupenda kwasababu ya utu wako, heshima yako mtaani na mahala popote unapokuwapo.

Kwa mfano, hata kama unahitaji kupendwa na mtu, kama mwonekano wako kwake ni vituko, nani anaweza kuweka chembechembe za upendo kwako, hasa wa kuishi kwa muda mrefu.
Badala yake, anaweza kuwa na wewe kwa muda tu, hasa kwa wale wasichana wazuri wanaotamaniwa na kila mtu, ingawa katika kutamani huko si endelevu.
0712 053949
0753 806087


No comments:

Post a Comment