Pages

Pages

Sunday, April 28, 2013

Bondia wa kike nchini Tanzania Pendo asikitika kukosa wapinzani


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa Kick Boxing nchini, Pendo Njau, amesema ukimya wake unatokana na kukosa wapinzani katika mchezo huo kutokana na kukimbiwa na mabondia wake, jambo linaloathiri ngumi za mateke.
Bondia mahiri wa kike nchini Tanzania, Pendo Njau
Akizungumza hivi karibuni kwenye Ukumbi wa mazoezi wa bondia Japhet Kaseba, Pendo alisema kinachoendelea ni mateso kwa mabondia wa kike hasa wale wanaotegemea mchezo huo.

Alisema mchezo huo kwa akina dada umezidi kuwa adimu, jambo ambalo linaweza kuangusha tasnia nzima, endapo juhudi za makusudi hazitachukuliwa kwa ajili ya kuhamasisha ngumi.

“Mimi ni bondia ambaye licha ya kuwa na malengo makubwa ya kuwika ndani na nje ya nchi, lakini nashindwa kutimiza ndoto kwasababu ya kukosa wanawake wenye moyo kama wangu.

“Hali hii inanifanya nione umuhimu wa kuwekeza nje zaidi, japo najua inaweza kuchukua muda kwasababu hata hao nao huangalia rekodi za bondia katika nchi yake kabla ya kugeukia Kimataifa,” alisema.

Pendo anatokea katika mikono ya Kaseba ambaye baada ya kuona ushindani kwenye Kick Boxing umetoweka, aliamua kuhamia kwenye masumbwi na kuleta upinzani wa hali ya juu.

No comments:

Post a Comment