Pages

Pages

Sunday, April 28, 2013

Afariki kwa kukanyagwa na gari mkoani Morogoro baada ya kudondoshwa na mwenzake

 
Mwili wa marehemu, Romanus Masige mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro ukiwa umelala chini katika barabara ya Old Dar es Salaam eneo la maktaba ya mkoa wa Morogoro baada ya kudaiwa kusukumwa na wenzake waliokuwa nao wamepakiwa nyuma ya lori wakati wakisafiri kutoka Kihonda kuelekea kituo kikuu cha polisi mjini hapa.(Picha zote kwa hisani ya Jackson Audiface

Shuhuda akieleza tukio zima lililotokea
Mwili wa marhemu Masige ukiwa umefunikwa kwenye eneo la tukio
Mwili wa marehemu ukipelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi
Hili gali ndilo lililomkanyaga marehemu
Msamalia akimwaga mchanga kwenye damu ya mtu aliyekanygwa na gari
.......................
Mashuhuda ambao walishuhudia tukio hilo walitudokeza kuwa nyuma ya lori hilo ilikuwa imebeba kokoo na abiria wawili na mara baada ya kufika eneo hilo alionekana moja wao akimsukuma marehemu aliyedondoka chini na gurudumu la nyuma lilimkanyaga na kupoteza maisha papo hapo huku mwenzake baada ya gari kusimama alichukua baiskeli na kutoweka eneo wakati dereva akijisalimisha kituo cha polisi.

"Alikanyagwa kichwani huyu marehemu na hilo lori baada ya kusukumwa na mwenzake na gari iliposimama alichukua baiskeli na kutoweka eneo hilo hatukuwezakuelewa nini kinaendelea". Kilisema Chanzo chetu.

Habari hizi kupitia blog hii iliendelea kudokezwa kuwa mkasa huo kwa marehemu huyo ulitokana na kitendo chake cha kupiga bosi wake kuuziwa kokoto hizo mara mbili jambo ambalo hakukubaliana nalo na kuwaona wahusika waliopeleka kokoto hizo kuwashuku kuwa ni wezi ndipo safari ya kuwapeleka kituo kikuu cha polisi na kabla hajafikiwa kituo tukio hilo likatokea majira ya saa 10 jioni jana.

Marehemu Masige ni mkazi wa Kihonda akiwa ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma ambapo taarifa zilizotufikia punde zinasema kuwa mwili wa marehemu huyo utasafirishwa kwa ajili ya mazishi mkoani Kigoma.

Masigealikuwa Mwali wa kwaya katikan kanisa katoliki kigango cha kristo mfalem na mlinzi katika kanisa hilo.

Mungu ailaze mahala pema peponi Amina

No comments:

Post a Comment