Pages

Pages

Sunday, April 28, 2013

Handeni Kwetu Blog yadhamini Redds Miss Kibaha 2013


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADHAMINI kibao wameendelea kumiminika katika Shindano la kumtafuta malkia wa Redds Miss Kibaha 2013 linalotarajiwa kufanyika baadaye mwezi ujao, huku mke wa Mbunge wa Kibaha, mama Celina Koka, Handeni Kwetu Blog na Multichoice nao wakijitokeza kuliwezesha shindano hilo.
Mmiliki wa Handeni Kwetu Blog, Kambi Mbwana

Shindano hilo linaloendelea na maandalizi yake ikiwapo kufanya mazoezi kabambe kwa warembo, pia linadhaminiwa na Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Blog, Handeni Kwetu Blog, The African Stars Entertainment (ASET) na Redds Premium Cold.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Linda Media Solution (LIMSO), Khadija Kalili, alisema kujitokeza kwa wadhamini hao ni sehemu ya kuliweka shindano lao kwenye kiwango cha juu.

Alisema amekuwa akiwaomba wadau hao wajitokeze kumsaidia ili kupatikana kwa mrembo mwenye kiwango cha juu kwa ajili ya kuleta ushindani katika tasnia ya urembo.

“Nashukuru kwa wadau wanaojitokeza kudhamini Miss Kibaha mwaka 2013 huku Linda ikiandaa kwa  mara ya kwanza, jambo linalonifanya niamini kuwa mambo yatakwenda sawa.

“Naamini mambo yatakuwa mazuri, ukizingatia kwamba tumekuwa kwenye mikakati kabambe, huku kila mshiriki akijua amefuata nini katika kinyang’anyiro hicho cha urembo,” alisema.

Kutokana na mikakati hiyo, waandaaji wa Miss Kibaha wameamua wafanye mazoezi katika Ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni, huku upande wa shoo ikiongozwa na mcheza shoo maarufu wa bendi ya Victoria Sound, Bokilo mwenye mchango mkubwa katika tasnia ya urembo kutokana na kusimamia shoo mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment