Pages

Pages

Thursday, April 25, 2013

TFF yapangua tena ratiba ya Ligi kati ya Simba na Ruvu Shooting iliyopangwa kufanyika leo Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Ruvu Shooting na Simba iliyokuwa ichezwe leo (Aprili 25 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 5 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
                         Boniface Wambura, Msemaji wa TFF
Mabadiliko hayo yametokana na Serikali kuutumia uwanja kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za Muungano ambazo kitaifa zitafanyika kesho (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kupitia msemaji wao Boniface Wambura, linawaomba radhi washabiki kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na mabadiliko hayo na ghafla. Ratiba ya mechi nyingine za VPL zinabaki kama zilivyo.

Ligi hiyo inaendelea kesho (Aprili 26 mwaka huu) kwa mechi kati ya Coastal Union na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Jumapili (Aprili 28 mwaka huu) itakuwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Simba dhidi ya Polisi Morogoro.

No comments:

Post a Comment