Pages

Pages

Sunday, April 28, 2013

Pitia maoni ya Mwanachama wa CCM, Hussein Bashe juu ya suala la Jimbo la Nzega na kukamatwa kwa Godbless Lema jijini Arusha



                          Mwana CCM Hussein Bashe
Ndg zangu, Awali ya yote niwatakie Juma pili njema na Kwa Ndg zetu wanoenda kanisani siku ya Leo waendelee kuombea Taifa letu na Viongozi wetu kufanya maamuzi ya busara juu ya Hatima ya Maisha ya Watanzania na Taifa kwa Ujumla.

Nimeanza na maneno hiyo hapa juu kufatia matukio miwili,Moja ni Tukio la Arusha na Pili ni Tukio la Maamuzi ya Baraza la Madiwani la wilaya ya Nzega.

Nzega
Halmashauri ya wilaya nzega imepitisha Bajeti na mipango ya Mendeleo ya mwaka wa fedha 2013/4 kilichonisikitisha ni Madiwani kujitengea milioni 82 kwa ajili ya ziara Kwenda mkoa ya Arusha, Dodoma Kama ziara ya kujifunza,Wakati wilaya inakabiliwa na Changamoto za uharibifu wa miundo mbinu kufatia muda Nyingi, makazi ya wananchi wengine yameharibika, shule za msingi na secondaries hazina Madawati, waalimu hawana nyumba, vituo vya Afya having dawa za kutosha, tunakabiliwa na tatizo la Maji Mijini na vijijini.

Wakati Hali ikiwa hivi fedha hizo ni Intrest(RIBA) iliyotokana na fedha zilizowekwa benki Baada ya mgodi kutulipa 2bn, Wabunge wakiwa wajumbe wa kamati ya fedha wamepitisha hili,mbali hapo wameunda tume ya Watu 15 Kwenda Dar kukutana na Katibu mkuu aw Nishati kufatilia madai Kila mjumbe atapewa posho ya siku 80,000 kwa siku 10 mbali na posho za madereva kwani wataondoka na gari za halmashauri, mbali na mafuta, kuna tume ya kufatilia mji mdogo nayo inawajumbe 10 imetengewa mamilioni ya pesa.

Mbali na Hilo wakubwa wameamua kumchukua fedha 2bn kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Nzega ikiwa na dhamira ya kutoa mikopo kwa Wananchi aw Nzega,wanafanya maamuzi haya huku wakifahamu Halmshauri ya wilaya ya Nzega Ina Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko aw Maendeleo ya Kina Mama, Mabilioni ya Jk vyote hivi vimeshindwa kusimamiwa na Fedha zake kwa Miaka yote hazijawahi kuwa na Mrejesho chanya Leo tena wanatenga fedha ili kuanzisha Benki itakayoendeshwa na Watu wale wale, kwa Mfumo ule ule, kuwakopesha Watu wale wale ambao Mara zote wanaposhindwa kurejesha hutumika sasa zile zile kuwasamehe.

Huu ni mchezo kwenye maisha ya wananchi aw wilaya ya nzega ambao hawana High school ,hawana barabara za uhakika,waalimu hawana makazi, wanafunzi hawana maabara,hawana Madawati, zahanati hazina Madawa, mikopo ya Mabilioni ya Jk haikufanikiwa, mikopo ya Mfuko wa Maendeleo wa Vijana haikufanikiwa, mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Kina mama haikufanikiwa Leo zinatengwa fedha za kuanzisha Benki ya kukopesha wana nzega, kuna Mabenki mawili nzega, kuna taasisi za mikopo zaidi 5 kwa matatizo yanayokabili wilaya lie huu ni Kupoteza fedha za wananchi wa nzg kwa posho na kuandaa maradi ambayo haina Tija.

TUKIO LA ARUSHA.
Tukio la kuuwawa Kijana aw Chou cha uhasibu na matokeo Yake badala ya kutafuta wauwaji kunatengenezwa mazingira ya kuleta Instabillity kwa kumkamata LEMA, Kaka yangu Mulongo katika hili alivolisimamia na kulitekeleza ameonyesha Udhaifu aw Hali ya Juu na matokeo Yake inavunjia heshima Serekali ya Chama chetu na Kuongeza chuki dhidi ya CCM Hakukua na sababu ya Kubahave the way he did pale chuoni,alionyesha kiburi hakua humble,hakutumia Busara katika jambo hili.

Wakati kuna Kijana ameuwawa,na yeye ndie Rais wa eneo lile attitude alionyesha Hakukua na leadership pale,tunakabiliwa na uchaguzi kuna mtu ameuwawa na si Tukio la kwanza, Nguvu iliyotumika kumkamata Lema Leo CCM mkoa aw Arusha wanakabiliana na maswali mengi kuliko Majibu, inasikitisha viongozi wanaotuwakilisha kuongoza ndio hao tunawaona Bungeni, ndio hao Kina Mulongo na maamuzi na attitude ya kaka Mulongo, ndio hao Kama Baraza la Madiwani wa Nzega ambao kwao semina safari, posho, maradi isiyotekelezeka, kuunda tume ya kuchunguza madai ya wafanyakazi ni kuitengea fungu Wakati Bajeti wameisha tenga fedha za kulipa madeni halafu unaunda tume ya kuchunguza madeni ambayo umeisha lipa.

Ndg zangu wana CCM chuki za Watanzania dhidi ya chama chetu zinaongezeka Kila siku na hii ni kutokana na Tabia zetu wenyewe Wakati hospitalini hakuna Vifaa vya Kina mama kujifungulia sisi tunajitengea fedha za ziara 82m,posho za 80,000 kwa siku,tunaanzisha miradi ambayo haitawasaidia wananchi kk kero zao za Kila siku,Wakati mwanafunzi ameuwawa na kibaka tunatumia mabomu,Rundo la Askari kumkamata mtu Moja kwakua si mwana CCM, wananchi nyumba zimebomolewa na mvua, hakuna Bajeti ya kuwasaidia hawa Watu, hakuna Madawati, dawa hospitali, tunaelekeza fedha ktk mambo yasiyogusa maisha Yao.

Unless tubadilike na kuanza kutambua Watanzania hawajatupa madaraka ilituchezee maisha Yao, unless tutambue uongozi ni dhamana tutendelea kuchukiwa na Leo sitashangaa Arusha tukipoteza kata 4 zilizowazi, tunawalazimisha Watanzania kutafuta matumaini kwa wapinzani kwa sisi wenyewe kuamua kujipa Utawala badala ya Uongozi.

Binafsi swala la nzega nimekiandikia Barua chama changu wilayan kukiomba kutazama upya maamuzi ya Full Council na kutambua upya vipaumbele halmashauri ya nzg inakabiliwa na Changamoto Nyingi hawatakiwi kuchezea fedha za walipa kodi. Hili la Arusha CCM inatakiwa kutolishabikia RC amemishandle the whole thing.

Haya ni maoni ya Hussein Bashe, mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM. Kumbuka, hayajaongezwa wala kupunguzwa, yakiwa na lengo la kufikisha ujumbe wake kwa Watanzania.

Mwaka 2010 aliwania kuteuliwa nafasi ya kugombea Ubunge Jimbo la Nzega, mkoani Tabora na nafasi hiyo kunyakuliwa na Dk. Hamis Kigwangwala kwa tiketi ya CCM.

No comments:

Post a Comment