Pages

Pages

Sunday, April 28, 2013

Redds Miss Kibaha wahamishia mazoezi yao Vijana Kinondoni


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki katika shindano lijalo la Redds Miss Kibaha 2013, wameanza kufanya mazoezi katika Ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni.
Baadhi ya warembo wa Miss Kibaha, wakiwa mazoezini

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO), ambaye pia ndio Mratibu wa shindano hilo Khadija Kalili, alisema warembo hao wamekuwa wakijifunza mbinu mbalimbali kwa ajili ya kulifanya shindano lao liwe na msisimko wa aina yake.

Alisema kuwa mwitikio wa warembo ni mkubwa, ndio maana wameamua kuweka mkazo katika suala zima la mazoezi ili mabinti wawe kwenye kiwango cha juu.

“Warembo wanaofanya mazoezi chini ya wakufunzi wao Sweat Ray na Bob Rich ni Nzeran Kitano, Martina Kapaya, Asma Said, Maud Bernad, Flora Mlowola na Nancy James.
 
Wengine ni Esther Albert, Beatrice Bahaya, Jenipher Njabiri na  Rachel John ambao wote kwa pamoja wanafundishwa shoo na mcheza shoo wa Victoria Sound, Bokilo,” alisema Khadija.
 
Kalili anawataja baadhi ya wadhamini waliojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Michuzi Blog, Handeni Kwetu Blog, The African Stars Entertainment (ASET) na Redds Premium Cold.

No comments:

Post a Comment