Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akizungumza jambo wakati wa kuchezesha droo ya saba ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10 ambapo bwana Sospeter Muchunguzi wa Ubungo, jijini Dar es Salaam alitangazwa mshindi.
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
DROO ya saba ya mchezo wa
Kubahatisha wa Biko, Ijue Nguvu ya Buku imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam,
huku Sospeter Muchunguzi akifanikiwa kuibuka kidedea na kuzoa Sh Milioni 10.
Mkazi huyo wa jiji
alifanikiwa kujinyakulia zawadi hiyo ya juu ya Sh Milioni 10 kutoka Biko,
katika droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa ushirikiano na
Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe.
Akizungumza katika droo hiyo
ya saba, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba Watanzania
wameendelea kupata hamasa kubwa na kujitokeza kwa wingi kuwania zawadi
mbalimbali za fedha taslimu kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000,
500,000 na Sh Milioni 1,000,000.
Kajala Masanja akionyesha namba ya mshindi.
“Ni furaha kwetu kuona idadi
kubwa ya Watanzania inajitokeza kwa wingi kucheza Biko na kupata zawadi
mbalimbali kutoka kwetu kwa kucheza bahati nasibu yetu kwa kufanya miamala
kuanzia Sh 1000 ambapo kwenye namba ya kampuni wataingiza 505050 na namba ya
kumbukumbu ni 2456.
“Biko bado inaendelea
kuchanja mbuga ambapo sasa tutakuwa tunachezesha droo kwa siku ya Jumatano na
Jumapili kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kila mtu anaibuka na ushindi wa Biko
na kuzoa mamilioni kutoka kwenye bahati nasibu yetu,” Alisema Heaven.
Naye Msimamizi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe, aliwataka Watanzania kuendelea
kuchangakia zawadi za Biko kwa kucheza kwa wingi kutokana na utaratibu mzuri na
urahisi wa mchezo wa Biko.
“Bodi yetu ipo makini
kufuatilia kwa kina uchezaji wa bahati nasibu, hivyo tunawaomba watu wacheze
kwa sababuBiko ni mchezo salama na unafuata kanuni, sheria na taratibu zote,”
Alisema Chiku ambaye pia aliwaasa akina mama kujitokeza kwa wingi ili nao
washinde mamilioni ya Biko.
Akizungumza kwa simu, mshindi
huyo wa droo ya saba ya Biko, Sospeter Muchunguzi, alishukuru kwa kuibuka na
ushindi huo, akisema ni mchezaji mzuri wa bahati nasibu hiyo ambapo mbali na
kushinda Sh Milioni 10, pia amewahi kushinda zawadi za papo hapo mara kadhaa.
Baada ya kutangazwa mshindi
wa Sh Milioni 10, Biko watamkabidhi mshindi huyo fedha zake mapema wiki hii
kama walivyokabidhiwa wengine ili waziweke katika mipango yao ya kimaisha.
No comments:
Post a Comment