Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela akizungumza wakati wa kufungua warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni mwenyekiti wa warsha akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela mara baada ya ufunguzi wa warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Na Mathias Canal, Dar es salaam akiteta jambo na Meya wa Manispaa ya kinondoni Mheshimiwa Benjamini Sitta ambaye pia ni
mwenyekiti wa warsha wakati wa warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028. Leo
Mei 11, 2017 Katika Ukumbi wa Hazina Mjini Iringa
Na Mathias Canal, Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela amefungua warsha
ya siku tatu ya kuwajengea wadau uelewa wa pamoja kuhusu programu ya
kuendeleza sekta ya kilimo Awamu ya pili nchini Agricultural sector
Development Programme (ASDP 2), Programu inayotarajiwa kutekelezwa
katika kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2027/2028.
Alisema kuwa ili kukuza na kuendeleza sekta ya kilimo nchini wataalamu
wote nchini wanapaswa kubadilishana ujuzi na kushauriana namna ya kuwa
na kilimo chenya tija kuliko kuficha ujuzi walionao kwa muktadha wa
maeneo husika pekee waliyopo hivyo ni vyema kutumia ujuzi wao kwa
makubaliano na maelekezano kwani jambo hilo litachochea zaidi ukuzaji wa
sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Dc Kasesela ameyasema hayo wakati
Akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo inayofanyika katika Ukumbi wa
Hazina Mjini Iringa, warsha inayowahusisha Makatibu Tawala wasaidizi
upande wa uchumi kutoka mkoa wa Iringa na Pwani na Maafisa kilimo wa
mikoa, Meya wa Manispaa/Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa
halmashauri za Manispaa/wilaya, Wachumi wa Manispaa/Wilaya na Maafisa
Kilimo wa Manispaa/Wilaya kutoka Katika Halmashauri za Manispaa na
Wilaya kutoka Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Dc Kasesela ameeleza
kuwa Programu hii ya ASDP 2 imeandaliwa baada ya kukamilika kwa awamu ya
kwanza ya ASDP 1 iliyotekelezwa kuanzia mwaka 2006/2007 hadi 2013/201
huku akiwapongeza waandaaji wa warsha hiyo ambao ni OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kutaraji
kutekelezwa na wadau mbalimbali kama vile Wizara za sekta ya kilimo,
Wahisani, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima
Wafugaji, na Wavuvi.
Dc Kasesela amesema kuwa Utekelezaji wa ASDP 2
utazingatia malengo ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano (2016-2021),
Mkakati wa Taifa wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Dira ya maendeleo
ya Tanzania (2025).
Alisema kuwa Programu hiyo imezingatia
vipaombele vya vizara ya Kilimo, Ufugaji na uvuvi na imelenga kutatua
changamoto na kuchochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo, Kuongeza pato
la Taifa, Kuboresha kipato cha wakulima wadogo na usalama wa chakula na
lishe nchini.
Sambamba na hayo pia alisema kuwa wadau wote wa ASDP 2
wanapaswa kusimamia na kutekeleza kwa weledi maeneo makuu manne ya
utekelezaji wa Programu hiyo ambayo ni Usimamizi wa Matumizi ya maji na
ardhi (Sustainable Water and Land use Management),, Kuongeza tija na
faida katika kilimo, mifugo na uvuvi (Enhanced Agricultural productivity
and profitability).
Maeneo mengine ya kusimamiwa vyema na wadau ni
Biashara na Uongezaji wa thamani kwenye mazao (Commercialization and
Value Addition, na Viwezeshi vya sekta, Uratibu, Ufuatiliaji, na
Tathmini ya sekta (Sector Enablers, Coordination and Monitoring and
Evaluation).
No comments:
Post a Comment