Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
BAHATI Nasibu ya
Biko Ijue Nguvu ya Buku, sasa imezidi kuchanja mbuga baada ya kuongeza donge
nono la washindi wa droo zao kubwa, ambapo sasa mshindi wa droo ya Jumatano hii
anatarajiwa kunyakua jumla ya Sh Milioni 20.
Mbali na kutoa
kiasi hicho cha pesa, tayari imempata mshindi wake wa droo ya tisa ya Jumapili
ambaye ni Leopard Mpande wa jijini Arusha, aliyenyakua Sh Milioni 10 huku pia
Biko ikiwa imeshapata washindi zaidi ya 35,000 wa papo kwa hapo.
Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo kushoto akiandika dondoo za mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko aliyetangazwa leo jijini Dar es Salaam, ambapo mkazi wa Arusha, Leopard Mpande aliibuka kidedea katika droo hiyo.
Akizungumza
leo katika droo iliyompata Mpande, Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko,
Grace Kaijage, alisema kwamba wameamua kuongeza zawadi ya droo kubwa ya
jumatano hii kutoka Sh Milioni 10 hadi 20 ili kuwawesha washiriki nafasi ya
kujikwamua kimaisha kwa zawadi za BIKO, "Changamkieni fursa hii"
alisema.
Alisema droo ya
kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 itafanyika Jumatano, huku akiwataka watu
wacheze mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za MPESA,
TIGOPESA na AIRTEL Money kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili au lipa kwa
MPESA ambapo watatakiwa waingize namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kuweka
pia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.
“Ukifanya hivyo
utaweka kiasi cha kununua tiketi kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo Sh 1000
itakuwa na nafasi mbili za ushindi kwenye droo kubwa ya Jumatano pamoja na
kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na sh 1,000,000, huku donge kubwa likipanda kutoka Sh Milioni
10 hadi 20 Jumatano hii.
“Biko ni kutoa
pesa kwa washindi wetu ili wafanikiwe katika maisha yao, hivyo wanachotakiwa
kufanya ni kucheza mara nyingi, huku pia nikimpongeza mkazi wa Arusha, ndugu
Mpande kufanikiwa kuibuka na Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa
Jumapili,” Alisema.
Naye Mwakilishi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo, aliwapongeza Biko kwa kufikia
hatua ya kutoa Sh Milioni 20 kwa washindi wa droo kubwa ya Jumatano akisema ni
hatua nzuri, hivyo Watanzania wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili waibuke na
mamilioni ya Biko.
“Sisi
tunafuatilia kwa karibu mchezo wa Biko na tunaridhishwa na utaratibu wao wa
upatikanaji wa washindi wa droo zao kubwa na ni mchezo wenye uaminifu mkubwa
hapa nchini ambapo wanatarajia droo ya Jumatano hii kutoa Sh Milioni 20, jambo
ambalo ni zuri kwa mustakabali wa kukuza uchumi kwa washiriki wote wa bahati
nasibu ya Biko,” Alisema Ngolo na kumpongeza pia mshindi wa Arusha aliyeibuka
na jumla ya Sh Milioni 10,” Alisema.
Kwa mujibu wa
Biko, droo ya Jumatano hii itatoa Sh Milioni 20, huku mshindi wao wa Arusha wa
Sh Milioni 10 akitarajiwa kukabidhiwa fedha zake haraka iwezekanavyo kama
walivyopewa washindi wengine walioshinda katika droo nane za Jumatano na
Jumapili zilizopita.
No comments:
Post a Comment