Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo, katikati akipokea fedha zake jumla ya Sh Milioni 10 alizoshinda katika bahati nasibu ya Biko katika droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyesimamia uingizaji wa fedha hizo katika akaunti ya Kapondo.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Droo ya Bahati Nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku
iliyochezeshwa juzi Jumatano, Stanley Kapondo, amekabidhiwa fedha zake jumla ya
Sh Milioni 10, huku akisema kuwa pesa hizo zimekuja wakati muafaka ili kuondoa
changamoto zinazomkabili katika maisha yake.
Makabidhiano hayo yamefanyika jana katika benki ya NMB jijini
Dar es Salaam kwa kusimamiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, ikiwa
ni siku moja baada ya kumpata mshindi wao wa droo ya Jumatano.
Mfanyakazi wa Shirika na Umeme TANESCO Stanley Kapondo
kushoto akifurahia fedha zake za ushindi wa droo ya Biko alizoshinda katika
droo ya Jumatano. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Kapondo alisema alikuwa
na uhitaji mkubwa wa pesa, hivyo aliamua kucheza Biko kama sehemu ya kutafuta
suluhu ya matatizo yake.
Alisema pamoja na kuamua kucheza Biko, hakuamini kwamba
angeshinda Sh Milioni 10, badala yake alikuwa anawazia ushindi wa Sh Milioni
moja aliyoona ni rahisi.
“Niliamua kuchezaa biko kwa kufanya miamala kwenye simu yangu
kwa kuweka namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kwenye namba ya kumbukumbu
niliweka 2456 kama wanavyohitaji ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio sababu
ya kutangazwa mshindi.
Pesa nilizopokea kutoka Biko si za kwanza maana nimekuwa
nikishinda zawadi za papo kwa hapo hadi Sh 50,000, hivyo binafsi nikajikuta
nawaamini zaidi Biko ukizingatia kuwa licha ya kuwahi kucheza bahati nasibu
nyingi, lakini kwa umri wangu wa miaka 52 sijawahi kubahatika,” Alisema Kapondo
ambaye pia ni mtumishi wa Shirika na Umeme Tanzania TANESCO, Ubungo.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka
Watanzania kucheza kwa wingi huku akisema zawadi za Sh Milioni 10 zitawaniwa
katika droo ya Jumatano na Jumapili huku zile za papo kwa hapo zikiendelea
kulipwa kwa kupitia simu za wachezaji wao.
“Biko imezidi kukolea, hivyo ni wakati wa kucheza mara nyingi
ili mjiwekee mazingira mazuri ya ushindi maana zawadi za papo kwa hapo kuanzia
Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatolewa
kila siku saa na kila siku, hivyo unachotakiwa ni kufanya miamala kwnye simu
zenu za Tigo, Vodacom na Airtel, huku tiketi ikipatikana kwa Sh 1000 au zaidi,”
Alisema Heaven.
Kwa mujibu wa Heaven, tiketi moja ya Sh 1000 itakuwa na
nafasi mbili ikiwa ni ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia
kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, watu wakishauriwa kucheza mara
nyingi zaidi ili wajiwekee mazingira mazuri ya ushindi wa Biko.
No comments:
Post a Comment