Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya nane iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu
ya Buku’ imefanyika huku mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan
Mwakaboko akifanikiwa kuibuka na mkwanja wa Sh Milioni 10.
Hiyo ni siku chache baada ya
wakazi wa Ubungo, Sospeter Muchunguzi na Stanley Kapondo, mfanyakazi wa
TANESCO nao kuibuka na mamilioni ya Biko kwa siku tofauti ndani ya wiki moja.
Akizungumza katika droo hiyo,
Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba siri kubwa ya ushindi ni kucheza
Biko mara nyingi zaidi, akiamini kuwa kila anayecheza ana nafasi kubwa ya
kuibuka kidedea na ushindi huo.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe kushoto akiwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja wakati wanamtafuta mshindi wa droo ya nane wa Biko ambaye mkazi wa Tabata, Daniel Mwakaboko alitangazwa mshindi na kuzoa jumla ya Sh Milioni 10 atakazokabidhiwa jijini Dar es Salaam.
Alisema mchezo wa Biko ni
mzuri na rahisi kucheza kwake, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutumia nafasi
yake vizuri kwa kucheza bahati nasibu hiyo iliyojizolea umaarufu katika kipindi
kifupi baada ya kuanzishwa kwake.
“Hakuna njia ya mkato ya
kuweza kushinda donge nono la Biko badala yake dawa ni kucheza kwa wingi kwa
kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuingiza namba ya
kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Kajala.
Naye Meneja Masoko wa Biko,
Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuingia kwa wingi katika mchezo wa Biko
hususan wakazi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania nao wakiwa kwenye nafasi kubwa
ya ushindi.
“Tumetoa zawadi kwa washindi
zaidi ya 30,000 nchi nzima kwa zawadi kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000,
100,000, 500,000 na Sh Milioni moja nchini kote, hivyo tunawaomba watu wa
mikoani nao kuongeza mwendo kuwania mamilioni ya Biko yanatotoka kila siku,
huku droo kubwa ya Sh Milioni 10 ikifanyika siku mbili kwa wiki, yani Jumatano
na Jumapili,” Alisema Heaven.
Naye Mwakilishi wa Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha Tanzania Chiku Salehe, alisema anajisikia faraja kuwa
mwangalizi katika droo iliyompa ushindi mkazi wa Tabata, Mwakaboko, akiamini
kuwa kila Mtanzania anaweza kuzoa mamilioni ya Biko.
“Mchezo wa Biko ni rahisi
kucheza, ni salama na tunaangalia kwa kina ili kila Mtanzania aweze kushinda
kihalali na kuongeza kipato chake kama walivyokusudia, ukizingatia kuwa endapo
mtu anaibuka na mamilioni ya Biko anaweza kufika mbali kiuchumi,” Alisema
Chiku.
Mshindi wa droo hiyo,
Mwakaboko hakusita kuonyesha furaha yake kwa kutangazwa mshindi, huku akisema
licha ya kuchelewa kushinda, lakini hakuvunjika moyo akiamini kuwa siku moja
bahati inaweza kuwa yake.
“Nashukuru sana kwa
kutangazwa mshindi wa Biko wa Sh Milioni 10, sasa nitaipata lini,” Alihoji
Mwakaboko kwa kupitia simu wakati anahojiana na balozi wa Biko, Kajala.
Kwa ushindi huo, Mwakaboko
anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake mapema ili aweze kuziingiza katika matumizi
yake ya kimaisha hususan ya kumkwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko
uliojizolea umaarufu mkubwa ukitambulika kama nguvu ya Buku.
No comments:
Post a Comment