Mkurugenzi Mtendaji wa Biko Tanzania Charles Mgeta mwenye miwani akishuhudia katika makabidhiano ya Sh Milioni 10 kwa mshindi wao wa jijini Arusha Leopard Mpande aliyepatikana katika droo ya Jumapili iliyopita. Aliyeshikana mikono na Mpande ni Balozi wa Biko Kajala Masanja.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAENDESHAJI
wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, jana wamemkabidhi zawadi yake
jumla ya Sh Milioni 10 mshindi wao wa jijini Arusha, Leopard Mpande,
aliyetangazwa mshindi katika droo ya tisa iliyofanyika Jumapili, jijini
Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko jijini Arusha, Leopard Mpande wa tatu kutoka kushoto akipokea nyaraka na fedha zake baada ya kukabidhiwa kutokana na ushindi wa droo ya nane ya Biko iliyochezeshwa Jumapili. Wengine wanaoshuhudia ni Balozi wa Biko, Kajala Masanja, Msanii Mpoki na maofisa wa NMB jijini Arusha.
Alisema wanajisikia faraja kubwa kuona watu wanaingia kwa wingi kucheza mchezo wao wa kubahatisha na kuzoa mamilioni ambapo zaidi ya Watanzania 35,000 wameshinda zawadi mbalimbali.
Mgeta
anasema hadi sasa wameshafanya droo kubwa tisa huku washindi wote wakiwa
wameshakabidhiwa fedha zao hivyo kufanya jumla ya Sh Milioni 90 kuwafikia
washindi wa droo kubwa za Sh Milioni 10.
Mshindi wa Biko jijini Arusha akisikiliza ushauri wa kifedha kutoka kwa afisa wa NMB Jijini Arusha jana.
“Huku
Jumatano ya kesho tukitoa Sh Milioni 20 kwa mshindi wetu wa droo kubwa,
tunajivunia kuona idadi ya wanaovuna mamilioni kutoka Biko inaongezeka kwa
kucheza kwa kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo jinsi ya kucheza
ni kufanya miamala kwenye simu zao kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni
505050 na kumbukumbu namba ikiwa ni 2456.
“Mtu anaweza
kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi huku kila tiketi moja inayopatikana kwa Sh
1000 ikiwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na nafasi ya
kuingia kwenye droo kubwa ya kuwania Sh Milioni 10, huku kwa Jumatano hii dau
likipanda hadi Sh Milioni 20,” alisema Mgeta.
Mgeta
aliongeza kuwa zawadi za papo kwa hapo zinazopatikana katika bahati nasibu yao
ni kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja
ambayo hulipwa kwa mshindi kwa kupitia simu yake aliyotumia kuchezea bahati
nasibu yao.
Naye Mpande
aliishukuru Biko kwa kumpa zawadi yake, akiamini kuwa kupokea kwa haraka
kumemfanya aamini kuwa Biko ni waendeshaji wa bahati nasibu za kisasa na zenye
uhakika mkubwa wa kushinda.
“
Nimepokea
zawadi yangu ya Sh Milioni 10 kwa furaha kwa sababu sikuamini kabisa kama
nimeshinda, lakini pia kama napokea fedha zangu kwa haraka kiasi hiki, ikiwa ni
siku moja baada ya kushinda kwenye droo ya Jumapili.
“Nawaomba
Watanzania wenzangu wasilaze damu, tuendelee kucheza Biko ili tuweze kuvuna
mamilioni kwa sababu njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi zaidi na tusikate
tamaa, ukizingatia kuwa hata mimi sikuamini kama naweza kutangazwa mshindi,”
Alisema.
Bahati Nasibu
ya Biko ni moja kati ya michezo iliyoibuka kwa siku za hivi karibuni na
kufanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa kutokana na utaratibu wake wa upatikanaji
wa washindi na kugawa zawadi kwa wakati jambo linalotafsiriwa kama fursa za
kiuchumi kwa wachezaji wake na Watanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment