Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akifurahia chakula cha asili ya Tanzania na mabalozi wa nchini nyingine katika maadhimisho ya Siku ya Afrika nchini hapa yaliyofanyika hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu, Riyadh
Balozi wa Tanzania UBALOZI wa Tanzania nchini Saudi
Arabia, uliungana na ofisi nyingine za balozi za nchi mbalimbali kusherehekea
Maadhimisho ya Siku ya Afrika yaliyofanyika hivi karibuni nchini Saudi Arabia.
Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba
na kutangaza utamaduni, ambapo kwa Tanzania, shamra shamra hizo zilikonga nyoyo
za wahudhuriaji wengi, ambapo wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini hapa
waliimba nyimbo za kuisifu na kuipamba Tanzania.
Wanafunzi
wa kitanzania baada ya kutumbuiza nyimbo za kuisifu Tanzania.Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, aliuambia Mtandao huu kuwa kusudio la kuungana na mabalozi wengine lilifanikiwa kwa sababu lengo halisi ni kuitangaza Afrika na nchi zao, ambapo anaamini kwa maadhimisho hayo nchi yake imepiga hatua kujitangaza kwa kuonyesha utamaduni wao kwa kupitia, ngoma, nyimbo, ngojera, maonesho ya mavazi na maonesho ya vyakula vya asili vya nchi zilizoshiriki,
Wakati wa Maakuli. Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akiwa ameshika sahani ya chakula katika maadhimisho ya Siku ya Afrika ambapo vyakula vya asili, ngoma na utamaduni wa Tanzania ulionyeshwa katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment