Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
MSHINDI wa droo ya nane ya
Bahati Nasibu ya Biko, ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Daniel Mwakaboko, jana amepokea
fedha zake jumla ya Sh Milioni 10, huku akisema kuwa zawadi aliyoshinda kutoka
kwenye bahati nasibu ya Biko itamkomboa kiuchumi na kumuondoa kwenye hatari ya
umasikini inayowakumba vijana wengi.
Akizungumza jana katika
makabidhiano ya fedha zake, Mwakaboko alisema kwamba zawadi ya fedha taslimu Sh
Milioni 10 ni nyingi kwa wakati huu anaposaka maisha bora kwa kutafuta mtaji
mara kadhaa bila mafanikio.
Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven kulia akimkabidhi jumla ya Sh
Milioni 10 mshindi wa droo ya nane ya Biko, Daniel Dancan Mwakaboko
aliyetangwa Jumatano ambapo jana alikabidhiwa fedha zake katika benki ya
NMB jijini Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa anafanya
kazi ya kuchapisha majarida na vitu tofauti tofauti vya kiofisi katika ofisi ya
mtu mwingine, hivyo ni wakati wake wa kuangalia namna gani atazitumia vizuri
fedha za ushindi alizokabidhiwa baada ya kuibuka na ushindi kartika droo ya
nane ya Biko iliyochezeshwa Jumatano.
“Biko ni mchezo mzuri
usiochosha na unaoweza kumpa kila mmoja wake ushindi kwa sababu hata uchezaji
wake wa kuweka muamala kwa simu za Tigo Pesa, MPESA na Airtel Money kwa kuanzia
Sh 1000 na kuendelea ni rahisi maana unachotakiwa ni kuingiza namba ya kampuni
505050 na kumbukumbu 2456 tayari kusubiri zawadi ya papo kwa hapo au droo kubwa
ya Sh Milioni 10.
“Nina ndoto ya kufanikiwa
kiuchumi lakini pia sitahasahau kiwanja maana vitu vyote hivi vilikuwa
vikisisumbua kwa siku nyingi na nadhani Mungu amejibu maombi yangu maana hapo
kabla hali yangu ilikuwa ngumu,” Alisema Mwakaboko mkazi wa Tabata na mwenye
asili ya mkoani Mbeya.
Naye Meneja Masoko wa Biko,
Goodhope Heaven, alisema kwamba kampuni yao imejipanga ipasavyo kuhakikisha
kwamba kila mtu anavuna mamilioni ya Biko kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000,
50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni Moja ambayo hulipwa papo kwa hapo dakika
chache baada ya mshindi kupatikana.
“Nawaomba Watanzania wote
bila kuangalia unapatikana eneo gani la Tanzania kucheza Biko mara nyingi zaidi
ili kujiwekea mazingira mazuri ya ushindi na kupata suluhu ya changamoto za
kimaisha kwa kupitia mchezo wa Biko maarufu kama Nguvu ya Buku,” Alisema
Heaven.
Meneja wa Huduma kwa Wateja
wa Biko, Grace Kaijage, alisema kwamba njia ya ushindi ni kucheza mara nyingi
zaidi ambapo pindi mtu anaposhinda hupewa zawadi yake kwa haraka, ambapo mpaka
sasa zaidi ya wateja 32000 wamepatikana na jumla ya Sh Milioni 80 zimelipwa kwa
washindi nane tu.
“Mpaka sasa tumefanya droo
kubwa za kuwania Sh Milioni 10 nane na tayari wateja wameshapewa stahiki zao
hivyo kuifanya Biko kutoa Sh Milioni 80 kwa washindi wake nane ukiacha wale
wanaolipwa papo kwa hapo ambao ndio wengi na wanatoka kila mikoa ya Tanzania,”
Alisema.
Droo kubwa ya kuwania Sh
Milioni 10 inayochezeshwa na Biko inafanyika mara mbili kwa wiki ambapo ni
Jumatano na Jumapili, huku mshindi wa zawadi za papo kwa hapo akipatikana kila
baada ya dakika chache.
No comments:
Post a Comment