Serikali kupitia Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga
nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya
askari wa jeshi hilo hapanchini.
Naibu
Waziri wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana
na Viongozi wengine kufungua Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na
wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa. Ufunguzi huo umefanyika
wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Akizungumzia changamoto
za makazi ya askari wa Jeshi la Magereza
Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali
inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika
mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba askari wetu nchi nzima wawe na subira Serikali inatambua na inashughulikia changamoto ya makazi ya askari na tayari tuko katika mazungumzo na
wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo
ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.
Awali akitoa maelezo ya
ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma
Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari
Magereza kwa kushirikiana na wafungwa kama
sehemu ya utekelezaji wa amri ya Mh. Rais
Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo
kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa Gereza hilo
umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano
wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa
ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka
wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.
No comments:
Post a Comment