https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, May 09, 2017

Mshindi wa MIlioni 10 Biko aahidi kuuaga umasikini

Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven mwenye fulana ya njano akionyesha nyaraka zilizowekwa kiasi cha Sh Milioni 10 kwa ajili ya mshindi wao wa wiki, Emmanuel Philipo aliyeibuka na ushindi wa mamilioni hayo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwa Heaven ni Philipo akifuatiwa na Afisa wa NMB na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa Biko IJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwake
wa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10. 

Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi, huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi wanaocheza bahati nasibu.

"Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko, hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050 na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa wiki.

Thursday, May 04, 2017

Balozi wa Tanzania Saudi Arabia atumia Sikukuu ya Muungano kutangaza Utalii

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.

Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia
SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
 Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam jana.

Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wameiptia bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili kuona vipau mbele vyake waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na ukubwa wake.

Kwa mwaka wa fedha wa 2016/ 2017 wizara hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni 845 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambayo tofauti yake sio kubwa.
 Mdau  Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.

RAS Tanga ataka waandishi wa habari kupewa ushirikiano

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Zena Saidi akifungua maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) leo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga, Lulu George.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo.

Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake

Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono ya shukrani na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven baada ya kumkabidhi fedha zake jijini Dar es Salaam kama sehemu ya ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko inayoendelea nchini Tanzania na kugawa mamilioni kwa washindi wake.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la mchezo bahati na nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limemkabidhi mshindi wake wa wiki ya tatu ya Sh Milioni 10, ambaye ni Pildas Emmanuel, anayeishi jijini Mwanza baada ya kutangazwa mshindi wa wiki katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.

Makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam sambamba na kumfungulia akaunti ya benki ya NMB kwa ajili ya kuingiza fedha hizo kwa mshindi huyo aliyejitambulisha kama mjasiriamali wa vileo jijini Mwanza Tanzania.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel aliyeletwa kwa Ndege kwa ajili ya kumkabidhi fedha zake.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kulia, akishuhudia jinsi mshindi wao wa Sh Milioni wa bahati nasibu ya Biko, Pildas Emmanuel anavyofurahia baada ya kumkabidhi fedha zake mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Na Mpiga Picha wetu.
 

Alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000, pamoja na zawadi kubwa ya wiki ya Sh Milioni 10 kwa kila mshindi wao, huku wakiwa wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili ambao ni Christopher Mgaya, Nicholaus Mlasu ambao wote wameshapokea fedha zao.

“Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri wananchi wa Watanzania wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa sh 1000.

Monday, May 01, 2017

Diwani wa Buzuruga mkoani Mwanza aongoza usafi Siku ya Wafanyakazi

Diwani wa Kata ya Buzuruga Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, Richard Machema (kushoto), akishiriki zoezi la usafi pamoja na Wananzengo wengine wa Kata hiyo katika Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.
BMGHabari
Wananzengo wa Kata ya Buzuruga wakiwa pamoja na diwani wao, Richard Machema (mwenye kofia), katika zoezi la usafi kwenye Kituo cha Afya Buzuruga hii leo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, 2017.

Mkazi wa Mwanza aibuka na mamilioni ya Biko



Msanii nyota wa filamu Tanzania, ambaye pia ni balozi wa Biko, Kajala Masanja, akionyesha namba ya ushindi wa Sh Milioni 10 aliyoshinda mkazi wa Mwanza, Pildas Emmanuel katika mchezo wa kubahatisha unaoendeshwa na Kampuni ya Biko Tanzania. Droo hiyo ilichezeshwa jana, jijini Dar es Salaam. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Mwanza, Pildas Emmanuel ameibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano la ‘Ijue Nguvu ya Buku’ katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na msimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha  Tanzania, Abdallah Hemed.

Droo ya bahati nasibu hiyo inayoendeshwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi katika simu za mikononi kupitia huduma za Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa ambapo pia ilichezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biko Tanzania, Charles Mgeta, alisema kwamba droo hiyo imeshirikisha washiriki zaidi ya 10,000 Tanzania nzima na kufanikiwa Emmanuel kutoka Mwanza kunyakua fedha hizo na kuingia katika historia ya mshindi wa kwanza kutoka mkoani.

Alisema Biko wamefurahia kuona mshindi wa droo ya tatu ametoka mkoani, baada ya droo mbili za awali ambazo zote washindi wake walitoka jijini Dar es Salaam kwa Christopher Mgaya na Nichoulas Mlasu kuibuka na Milioni 10.

“Tunawapongeza washiriki wote wanaogombania gurudumu la mchezo wetu wa Biko ambao umeshika kasi, huku nikimpongeza pia mshindi wetu wa mkoani Mwanza, Emmanuel kuibuka na ushindi huu ambao kwa hakika unaweza kubadilisha maisha yake.

Wednesday, April 26, 2017

EFG yapongezwa kufungua klabu za kupinga ukatili jijini Dar es Salaam

 Mfanyabiashara wa nguo za mitumba ya kike katika Soko la Ilala Boma jijini Dar es Salaam, Daud Omary (kushoto), akitoa maelezo Dar es Salaa jana ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa na baadhi ya askari polisi wa Kituo cha Pangani kwa Mwezeshaji wa kisheria katika soko hilo (kulia) kutoka Shirika la Equality for Growth (EfG), wakati wa uhamsishaji wa kufungua klabu za mabadiliko ya kupinga ukatili wa kijinsia masokoni unaofanywa na Shirika hilo kwa kusimamiwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake Tanzania (WLAC) kupitia kampeni ya miezi miwili ya  Tunaweza. Katikati ni mfanyabiashara Seleman Adam.

 Fundi ushonaji nguo katika Soko la Ilala Boma, Abdallah Omari (kulia), akitoa maelezo kwa mwezeshaji sheria kutoka Shirika la EfG, Aisha Juma wakati wa kujiunga na klabu ya mabadiliko ya wapinga ukatili wa kijinsia.

Milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’ zamfikia Nicholaus Mlasu wa Ukonga

Ofisa wa benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam kushoto, akimkabidhi moja ya karatasi muhimu baada ya kufanikiwa kumfungulia akaunti mshindi wa Biko, Ijue Nguvu ya  Buku, Nicholaus Mlasu aliyeibuka na ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko mwishoni mwa wiki. Makabidhiano ya fedha za ushindi huo yalifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Picha zote na Mpiga picha Wetu.



Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ZAWADI ya juu ya Sh Milioni 10 inayotolewa na Bahati Nasibu ya Biko, Ijue Nguvu ya Buku imetolewa jana na kukabidhiwa mshindi Nicholaus Mlasu, mkazi wa Ukonga Mombasa, Manispaa ya Ilala, huku akipokea fedha zake Makao Makuu ya Benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.

Fedha za mshindi huyo ziliingizwa moja kwa moja kwenye akaunti yake iliyofunguliwa kwenye benki hiyo kwa ajili ya kijana huyo kujipanga vizuri kabla ya kuanza kuzitumia fedha hizo kwa maendeleo yake.
Meneja Masoko wa Biko Tanzania waendeshaji wa Bahati Nasibu kwa njia ya ujumbe wa maneno kwenye simu za mikononi, Goodhope Heaven kulia akizungumza jambo wakati wa kumfungulia akaunti mshindi wao wa Sh Milioni 10 na kumkabidhi fedha hizo jana Makao Makuu ya benki ya NMB, jijini Dar es Salaam. Katikati ni mshindi huyo Nicholaus Mlasu akifuatiwa na Ofisa wa NMB Makao Makuu. 

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema kwamba mbali na kutoa fedha hizo kila mwisho wa wiki, pia wanaendelea kutoa pesa za papo kwa hapo ambapo ongezeko la washiriki ni kubwa.


Alisema wale wanaoshinda papo hapo fedha kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja hupokea kwenye simu zao wanazotumia ambazo ni Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money, ikiwa ni baada ya kuingia kwenye kipengele cha lipa bili, kuingiza namba ya kampuni 505050 na kuingiza namba ya kumbukumbu 2456.

Sunday, April 23, 2017

Nicholaus Mlasu azoa milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’

 
Msanii wa nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja kulia, akichezesha droo ya pili ya kuwania Sh Milioni 10 ya mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko 'Nguvu ya Buku' iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wake Nicholaus Mlasu kutoka Ukonga Mombasa, Ilala alinyakua kitita hicho na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo mwenye kitabu mkoni. Katikati ni mshindi wa Biko wa wiki iliyopita, Christopher Mgaya. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Na Mandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya pili ya wiki kutafutwa mshindi wa shindano la Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ ya kuwania Sh Milioni 10 imefanyika leo asubuhi huku mkazi wa Ukonga Mombasa, Ilala, jijini Dar es Salaam, ameibuka na ushindi huo na kuwa mtu wa pili kufaidika na mamilioni ya Biko, baada ya Christopher Mgaya kushinda wikiiliyopita na kukabidhiwa mamilioni yake.
Picha nyingine Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Biko wa wiki hii Nicholaus Mlasu kunyakua Sh Milioni 10 za Biko katika droo hiyo.

Mshindi huyo amepatikana katika droo iliyochezeshwa jana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja pamoja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo pamoja na Mgaya mshindi wa wiki iliyopita.
Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania kwenye notebook mkononi pamoja na mshindi wa wiki iliyopita, Chiristopher Mgaya wakiisoma namba ya mshindi wa wiki hii ambaye bwana Nicholaus Mlasu alitangazwa mshindi.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni furaha yao kubwa kuona wamempata mshindi mwingine aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano lao linalofanyika kila mwisho wa wiki.

Alisema bahati nasibu ya Biko imezidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa siku chache kutokana na urahisi wake wa kucheza pamoja na kutumia muda mdogo kulipa washindi wake, hususan wa zawazi za papo kwa papo zinazopatikana baada ya kucheza kwa kufanya miamala ya kifedha kwa simu za Vodacom, Tigo na Airtel Money.

“Ni rahisi kucheza Biko kwa sababu mtu anafanya muamala kwenye simu yake kuanzia Sh 1000 ambapo kwanza katika kipengele cha lipa bili, atakwenda kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kisha ataweka 2456 kama namba yetu ya kumbukumbu.

Wednesday, April 19, 2017

Utalii wa kutumia Baloon wawa kivutio Hifadhi ya Taifa Serengeti

Kikapu maalumu kinachotumika katika Baloon kwa ajili ya kubeba watalii kikishushwa katika eneo la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya Utalii wa Baloon.
Waandaaji wa Baloon wakifanya maandalizi ya kuliandaa Baloon hilo kwa ajili ya kubeba wageni wakati wa maandalizi ya kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mshindi wa Biko Milioni 10 apokea fedha zake na elimu NMB

Ofisa wa Benki ya NMB kushoto akimkabidhi kadi yake ya benki mshindi wa shindano la bahati nasibu ya Biko baada ya kushinda Sh Milioni 10 za shindano hilo nchini Tanzania. Anayeshuhudia kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven. Makabidhiano hayo ya fedha na kadi ya benki kwa mshindi huyo yalifanyika Makao Makuu ya benki ya NMB kama sehemu ya kumuandaa mshindi wa Biko kuzitumia fedha zake kwa uangalifu ili zimnufaishe kiuchumi.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa shindano la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Christopher Mgaya, jana amepokea fedha zake sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka Benki ya NMB ambapo alifunguliwa akaunti ya kuhifadhia fedha hizo.

Mgaya alitangazwa mwishoni mwa wiki katika droo ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, droo iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo, jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akisikiliza wakati Meneja Masoko wa Biko Tanzania, wachezeshaji wa bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven, wakati anafanya mazungumzo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam. Fedha hizo alikabidhiwa jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake. 


Nia ya kufunguliwa akaunti katika tawi la NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam sambamba na kupatiwa elimu ya kifedha kwa mshindi huyo limetokana na kiu ya kumuandaa kijana huyo ili aweze kuzitumia ipasavyo fedha zake kwa ajili ya kumuinua kiuchumi kutokana na uwapo wa mchezo wa bahati nasibu huo unaochezwa kwa kufanya miamala ya kifedha kwenye Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money.

Monday, April 17, 2017

jinsi Sikukuu ya Pasaka ilivyosherehekewa jana jijini Dar es Salaam

 Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kivule, Dar es Salaam, wakiimba kwa hamasa wimbo wa kufufuka kwa Yesu Kristo wakati wa Ibada ya Pasaka leo. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Kwaya ya watoto ikiimba wimbo maalumu wa kufufuka kwa Yesu Kristo kanisani hapo jana.

‘Nguvu ya Buku’ yampatia Sh Milioni 10 Christopher Mgaya

Msanii nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja, kulia akishiriki katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku inayoendeshwa na Kampuni ya Biko ambapo ilimpata mshindi wake wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambaye ni Christopher Mgaya, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Juhudi Ngolo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya kwanza ya kuwania Sh Milioni 10 iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki imempatia donge nono mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya na kuweka historia ya kuwa mtu wa kwanza kujinyakulia kitita hicho kutoka kwa mchezo wa bahati nasibu wa Biko.

Droo hiyo ilichezeshwa na msanii nyota wa filamu nchini Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Juhudi Ngolo.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo kushoto akichezesha droo kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, ambapo mkazi wa Temeke, Christopher Mgaya aliibuka na kitita hicho. Kulia ni msanii wa filamu, Kajala Masanja, akishuhudia.


Akizungumza katika droo hiyo jana, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba jumla ya washindi 2000 walipatikana katika zawadi mbalimbali, huku Mgaya yeye akiibuka kinara wa Sh Milioni 10.


Heaven alisema kwamba baada ya kupatikana kwa mteja huyo, taratibu za kumkabidhi hundi yake ya Sh Milioni 10 unaweka ili mteja huyo apate fedha zake haraka iwezekanavyo.


“Tumeanza vizuri kwa kufanikiwa kumpata mshindi wetu wa kwanza wa Sh Milioni 10 ambapo alicheza bahati nasibu yetu, huku yeye akifanikiwa kuibuka mshindi.

Monday, April 10, 2017

Droo ya Milioni 10 ya nguvu ya buku kuchezeshwa Jumapili hii

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MCHEZO wa bahati nasibu unaoendeshwa na Biko, unaotambulika kama Ijue nguvu ya Buku unatarajiwa kuchezesha droo yake ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, Jumapili hii.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe (wapili kushoto), akimkabidhi Leseni  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta kwa ajili ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven. Picha zote na Mpigapicha Wetu.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya BIKO Charles Mgeta mara baada ya kupeana leseni ya kufanya shughuli za mchezo wa kubahatisha nchini unaoitwa kama Nguvu ya Buku. Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biko, Charles Mgeta, alipofanya mazungumzo na waandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo na kuhudhuriwa na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

Akizungumza katika mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mkuu Mgeta, alisema droo yao itakuwa ya kwanza tangu walipoanzisha mchezo huo wenye zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10000, 20000, 50,000, 200,000 na sh Milioni moja, huku zawadi ya Sh Milioni 10 ikipatikana kila mwisho wa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea leseni ya uendeshaji wa michezo ya kubahatisha kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, James Mbalwe wa pili kushoto. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Udhibiti wa Bodi hiyo Sadick Elimusu na Kulia ni Meneja Masoko wa BIKO Goodhop Heaven.

Friday, March 17, 2017

Rais Magufuli afuta agizo la vyeti vya Waziri Mwakyembe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU

Usambara Development yatoa msaada wa saruji wilayani Lushoto

 Wanafunzi wa shule ya secondari viti kata ya shume wilayani Lushoto wakipokea mifuko ya saruji yenye thamani ya shilingi laki tano kwa ajili ya ujenzi wa choo kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE (UDI) ikiwa ni katika kuchangia juhudi za Mh. Mbunge wa Mlalo mh. Rashid Shangazi za kuleta maendeleo jimboni hapo.
 Diwani wa kata ya Vuga wilayani Lushoto mh. Dhahabu jumaa akipokea miche ya miti kutoka kwa taasisi ya USAMBARA DEVELOPMENT INITIATIVE , ikiwa ni juhudi za kuendeleza na kutunza mazingira wilayani Lushoto, pichani anayekabidhi ni katibu Mkuu wa UDI DIckson shekivuli na naibu katibu Mkuu Frank shempemba.

Thursday, February 23, 2017

Jumia yazindua huduma za ndege

 Ofisa Habari wa Kampuni ya Jumia Travel, Geofrey Kijangwa (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu kampuni hiyo kuzindua huduma za ndege. Kushoto ni Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Fatema Dharsee. 

Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Jumia Travel imetangaza kuwa imezindua huduma za ndege kwa ajili ya wasafiri, hatua ambayo itapelekea kutanua wigo wa huduma zake. 

Uzinduzi huu unakuja kipindi ambacho Kilele cha Mkutano wa Pili wa Masuala ya Anga Afrika ukifanyika nchini Rwanda. 

Kwa sasa mtandao huo nambari moja kwa huduma za hoteli barani Afrika unatoa huduma za ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na mashirika makubwa ya ndege yakiwemo Precision Air, Kenya Airways, Rwandair Express, Qatar Airways, Emirates, Ethiopian Airlines, South African Airways, KLM, Fly Dubai, Turkish Airlines, Air Arabia, Air Seychelles miongoni mwa nyinginezo.
 Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo, Fatema Dharsee akizungumza na wanahabari.

TAYODEA yapongezwa kuinua uchumi wa vijana jijini Tanga

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim

 Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza.

Wednesday, February 22, 2017

Semina yakutanisha vijana mbalimbali kujadili changamoto zao


Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia  Global Peace Foundation (GPF) Tanzania aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi kuhusu Asasi hiyo.

Wajasiriamali watembelewa katika maeneo yao nchini Tanzania

Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim akiwa katika moja ya mikoa kukagua na kuimarisha shughuli za Wajasiriamali wanachama wa kampuni hiyo katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari hadi leo ameshafanya ziara katika mikoa ya Iringa, Tabora, Kigoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Mafunzo yanayotolewa na kampuni hiyo kwa wajasiriamali zaidi ya 400,000 nchini ni. ufugaji wa kuku wa chotara, sungura, samaki pamoja na kilimo bishara cha mbogamboga na matunda.

Pia husaidia kupatika kwa masoko ya bidhaa hizo, pamoja na kuwaunganisha katika taasisi mbalimbali za kifedha ili kupata mikopo kirahisi. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda.

Tuesday, February 21, 2017

Bayport yatoa kompyuta nne kwa shule za Msingi Dodoma Mjini

Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mvunde (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta Nne kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha Bayport Tanzania, Ngula Cheyo mjini Dodoma leo asubuhi. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa taasisi hiyo, Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa taasisi hiyo, Christopher Kihwele. 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imemkabidhi kompyuta nne Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mheshimiwa Anthon Mavunde kwa ajili ya shule za Msingi za Majengo, Chigonge, Mahomanyika na Uhuru zilizopo mjini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Majengo, wakinyoosha mikono juu katika tukio la kukabidhiwa kompyuta nne za Bayport Financial Services, zikipokewa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya Msingi Majengo, ambapo kompyuta hizo zina lengo la kuongeza kiwango cha elimu mkoani Dodoma. Akizungumza leo mjini Dodoma, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba msaada huo wa kompyuta umetokana na dhamira yao ya kusaidia jamii kwenye sekta ya elimu kama njia ya kuikomboa jamii.

Alisema kwamba si mara ya kwanza kusaidia sekta ya elimu kutokana na kujitokeza mara kadhaa kujenga madarasa, kununua thamani za shule pamoja na kudhamini mikopo ya elimu ya juu na vitabu. 
Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Majengo, wakisoma shairi mahususi kwa ajili ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana, Anthony Mavunde wakati anakabidhiwa kompyuta nne kutoka kwenye taasisi ya Bayport Financial Services.

“Bayport tuna lengo la kuikwamua jamii katika maendeleo kwa kuhakikisha kwamba tunakuza kiwango cha elimu, hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma, tumeamua kutoa kompyuta nne kwa kuboresha miundo mbinu ya elimu ili nchi yetu isonge mbele.

Monday, February 20, 2017

Mkuu wa wilaya Muheza ajionea zoezi la upasuaji wa macho Kituo cha Afya Ubwari

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiingia kwenye kituo cha Afya Cha Ubwari leo wakati alipokwenda kuangalia zoezi la upasuaji wa macho kwa wakazi wa wilaya hiyo wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya mtoto wa Jicho iliyoendeshwa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo,Mathew Mganga na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Luiza Mlelwa.



Baadhi ya wazee waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani
Baadhi ya wananchi waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani.

Mbunge wa Mkuranga aongoza tukio la kuchangia damu Dar es Salaam

Mgeni rasmi wa kongamano la kuchangia damu lililoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga akizungumza umuhimu wa kila Mtanzania kujitolea damu ili kuinusuru jamii yake. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, mwishoni mwa wiki aliongozana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), lililofanyika katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo, watu mbalimbali walishiriki katika uchangiaji damu kama sehemu ya kutatua changamoto ya upungufu wa damu kwa wenye uhitaji, wakiwamo akina mama wajawazito, ajali za barabarani na majanga mengine.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, H.E Jasem Al Najem akitolewa damu katika tukio la kuchangia damu lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam.


Akizungumza katika uchangiaji huo, Mbunge Ulega alisema kwamba jukumu la kuchangia damu linamuhusu kila Mtanzania, huku akiwataka watu kujenga mazoea ya kujitolea damu ili kuondoa upungufu wa damu.

Alisema kwamba mahitaji ya damu kwa nchi yetu ni makubwa, hivyo amefarijika kwa kupata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi sambamba na kuongoza tukio hilo la uchangiaji wa damu, akiamini amejitolea jambo la msingi na la lazima.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...