Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa shindano la bahati nasibu
ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Christopher Mgaya, jana amepokea fedha zake
sambamba na kupewa elimu ya kifedha kutoka Benki ya NMB ambapo alifunguliwa
akaunti ya kuhifadhia fedha hizo.
Mgaya alitangazwa mwishoni mwa wiki
katika droo ya kwanza ya kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, droo
iliyochezeshwa na Balozi wa Biko Tanzania, Kajala Masanja akishirikiana na mwakilishi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Juhudi Ngolo, jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akisikiliza wakati Meneja Masoko wa Biko Tanzania, wachezeshaji wa bahati nasibu ya Ijue Nguvu ya Buku, Goodhope Heaven, wakati anafanya mazungumzo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam. Fedha hizo alikabidhiwa jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake.
Nia ya kufunguliwa akaunti katika
tawi la NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam sambamba na kupatiwa elimu ya
kifedha kwa mshindi huyo limetokana na kiu ya kumuandaa kijana huyo ili aweze
kuzitumia ipasavyo fedha zake kwa ajili ya kumuinua kiuchumi kutokana na uwapo
wa mchezo wa bahati nasibu huo unaochezwa kwa kufanya miamala ya kifedha kwenye
Tigo Pesa, Mpesa na Airtel Money.
Ofisa wa NMB akimkabidh mshindi wa Biko kadi yake ya ATM ya benki hiyo tayari kwa matumizi yake.
Mshindi wa Sh Milioni 10 wa mchezo wa kubahatisha wa Biko, Christopher Mgaya, akipokea fedha zake alizoshinda baada ya kutangazwa mwishoni mwa wiki na kukabidhiwa mapema jana Makao Makuu ya NMB jijini Dar es Salaam sambamba na kupewa elimu ya kifedha ili fedha hizo zimnufaishe kiuchumi na kubadilisha maisha yake. Kulia kwake ni Meneja Masoko wa Biko Goodhope Heaven.
Akizungumza katika ufunguzi wa
akaunti ya mshindi wao huyo jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema
kwa mshindi wao wa Sh Milioni 10 wameona wasimuache hivi hivi badala yake
wakaamua kumfungulia akaunti NMB sanjari na kupatiwa elimu ya kifedha ili
zimuendeleze kimaisha.
“Biko ushindi ni nje nje kwa kuwa
lengo letu ni kuwafanya Watanzania wafanikiwe kimaisha kwa kuutumia vema mchezo
wetu huu kwa kuingia kwenye kipengele cha lipa bili kwenye simu zao za Mpesa,
Tigo Pesa na Airtel Money kisha kuingiza namba ya kampuni 505050 na kumalizia
namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456.
“Biko tunalipa kwa haraka kwa zawadi
za papo kwa hapo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na
sh Milioni moja, huku zawadi ya ushindi wa Sh Milioni 10 inayopatikana kwa
kuchezeshwa droo kila mwisho wa wiki italipwa kwa njia ya hundi na kumuingizia
fedha zake benki kama tulivyofanya kwa mshindi wetu Mgaya aliyeibuka na ushindi
kutokea Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,” Alisema.
Naye Mgaya alisema kwamba
anawashukuru Biko kwa kumpatia zawadi yake kwa haraka sambamba na kumpeleka NMB
ili apatiwe elimu namna gani atazitumia fedha hizo ili zimuendeleze badala ya
kuzitumia kwa matumizi yasiyokuwa ya lazima.
“Wakati nashiriki kucheza Biko
sikutaraajia kama ningeshinda, lakini baada ya awali kushinda pia Sh 5000,
nilihamasika na kuendelea kucheza ambapo Jumapili sikuamini baada ya kupigiwa
simu na Kajala akinitaarifu kuwa nimeshinda Sh Milioni 10, ushindi ambao hakika
utanitoa sehemu moja kwenda nyingine hususan kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba.
“Nawashukuru Biko huku
nikiwakumbusha Watanzania wenzangu kuchangamkia fursa ya bahati nasibu ya Biko
kwa sababu haiitaji kujua lolote zaidi ya kucheza kwa njia ya ujumbe wa simu na
kuingiza miamala kiasi cha Sh 1000 na kuendelea, huku kila Sh 1000 tunayolipa
ikitupatia nafasi mbili, zawadi za papo kwa hapo pamoja na nafasi ya kuingia
moja kwa moja kwenye droo ya kubwa ya wiki yakuwania Sh Milioni 10,” Alisema
Mgaya.
No comments:
Post a Comment