Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani
Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na
Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu
kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali
uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment