Msanii
wa nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja kulia, akichezesha droo ya pili
ya kuwania Sh Milioni 10 ya mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko 'Nguvu ya
Buku' iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wake
Nicholaus Mlasu kutoka Ukonga Mombasa, Ilala alinyakua kitita hicho na kuhudhuriwa na
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo
mwenye kitabu mkoni. Katikati ni mshindi wa Biko wa wiki iliyopita,
Christopher Mgaya. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Na Mandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO
ya pili ya wiki kutafutwa mshindi wa shindano la Bahati Nasibu ya Biko
‘Ijue Nguvu ya Buku’ ya kuwania Sh Milioni 10 imefanyika leo asubuhi huku mkazi wa Ukonga Mombasa, Ilala, jijini Dar es Salaam,
ameibuka na ushindi huo na kuwa mtu wa pili kufaidika na mamilioni ya
Biko, baada ya Christopher Mgaya kushinda wikiiliyopita na kukabidhiwa
mamilioni yake.
Picha nyingine Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Biko wa wiki hii Nicholaus Mlasu kunyakua Sh Milioni 10 za Biko katika droo hiyo.
Mshindi
huyo amepatikana katika droo iliyochezeshwa jana na Balozi wa Biko,
Kajala Masanja pamoja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha
Tanzania, Jehud Ngolo pamoja na Mgaya mshindi wa wiki iliyopita.
Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania kwenye notebook mkononi pamoja na mshindi wa wiki iliyopita, Chiristopher Mgaya wakiisoma namba ya mshindi wa wiki hii ambaye bwana Nicholaus Mlasu alitangazwa mshindi.
Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni furaha yao kubwa kuona wamempata mshindi mwingine aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano lao linalofanyika kila mwisho wa wiki.
Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni furaha yao kubwa kuona wamempata mshindi mwingine aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano lao linalofanyika kila mwisho wa wiki.
Alisema bahati
nasibu ya Biko imezidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa siku chache
kutokana na urahisi wake wa kucheza pamoja na kutumia muda mdogo kulipa
washindi wake, hususan wa zawazi za papo kwa papo zinazopatikana baada
ya kucheza kwa kufanya miamala ya kifedha kwa simu za Vodacom, Tigo na
Airtel Money.
“Ni
rahisi kucheza Biko kwa sababu mtu anafanya muamala kwenye simu yake
kuanzia Sh 1000 ambapo kwanza katika kipengele cha lipa bili, atakwenda
kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kisha ataweka 2456 kama namba
yetu ya kumbukumbu.
“Baada
ya kufanya hivyo mteja atapokea ujumbe wa maandishi katika simu yake
kumjulisha hatua aliyofikia baada ya kucheza na tunashauri wateja
wacheze biko mara nyingi ili wajiwekee nafasi nzuri ya kushinda kuanzia
Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Milioni 1,000,000
kama zawadi zetu za papo kwa hapo, pamoja kupata nafasi ya kuingia
kwenye droo ya wiki kuwania donge nono la Sh Milioni kumi (10,000,000)
ambalo leo ndugu yetu Mlasu ameibuka na ushindi huo mnono,” Alisema
Heaven na kumpongeza mshindi wao pamoja na kuwataka Watanzania
wajitokeze kwa wingi kuwania mamilioni ya Biko.
Naye
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo alisema
kwamba ni hatua nzuri kuona washindi wa Biko wanapatikana kila wiki
sambamba na kupokea zawadi zao haraka.
“Bodi
tunafarijika kwa sababu wale washindi wanapopatikana hupokea malipo yao
kwa haraka hivyo wanaweza kuzitumia fedha zao katika mambo ya
kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko, hivyo
nawaomba Watanzania waendelee kucheza biko ili wapate nafasi ya kuvuna
fedha mbalimbali kwa kupitia bahati nasibu ya Biko,” alisema.
Naye
mshindi wa Sh Milioni 10, Nicholaus Mlasu, alipokea simu ya ushindi kwa
furaha na kusema amefurahishwa kwa sababu alikuwa akicheza Biko kwa
malengo ya kushinda sambamba na kumuomba Mungu atimize maombi yake ili
azoe mamilioni ya Biko.
Nimefurahi
sana kwa kushinda Biko, namshukuru Mungu kwa kuniona maana sasa
nimeweza kuibuka na mamilioni hayo ambayo nitayatumia vizuri maana ndio
malengo yangu ya kucheza Biko kila siku ili niweze kushinda donge nono,
alisema Mlasu.
Bahati
nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku imezidi kushika kasi huku tayari ikiwa
imeshamkabidhi mshindi wake wa kwanza Christopher Mgaya Sh Milioni 10
zake wiki iliyopita sambamba na kupewa elimu ya fedha kutoka benki ya
NMB, Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment