Na Mwandishi
Wetu, Dar es Salaam
MBUNGE wa
Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, mwishoni mwa wiki aliongozana na Balozi wa
Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, katika tukio la uchangiaji wa damu
lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF),
lililofanyika katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam. Katika tukio
hilo, watu mbalimbali walishiriki katika uchangiaji damu kama sehemu ya kutatua
changamoto ya upungufu wa damu kwa wenye uhitaji, wakiwamo akina mama
wajawazito, ajali za barabarani na majanga mengine.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, H.E Jasem Al Najem akitolewa damu katika tukio la kuchangia damu lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika uchangiaji huo, Mbunge Ulega alisema kwamba jukumu la kuchangia damu
linamuhusu kila Mtanzania, huku akiwataka watu kujenga mazoea ya kujitolea damu
ili kuondoa upungufu wa damu.
Alisema
kwamba mahitaji ya damu kwa nchi yetu ni makubwa, hivyo amefarijika kwa kupata
mwaliko wa kuwa mgeni rasmi sambamba na kuongoza tukio hilo la uchangiaji wa
damu, akiamini amejitolea jambo la msingi na la lazima.
Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega, akizungumza na Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem wakati wanatoa damu kwenye tukio lililoandaliwa na TYPF mwishoni mwa wiki.Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem wakati anapima uzito dakika chache kabla ya kutoa damu katika tukio lililofanyika mwishoni mwiki.
“Nimefarijika
kwa mwaliko wenu na jinsi nilivyoshiriki juu ya utoaji wa damu nikiamini kwamba
naweza kusaidia wenye uhitaji wanapokuwa Hospitalini ambapo juu ya damu
inayohitajiwa kwa kiasi kikubwa ili kuwanusuru wagonjwa wetu,” Alisema Ulega na
kuwataka TYPF kuelekea jimboni kwake Mkuranga kwa ajili ya kuandaa matukio ya
aina hiyo ili waendeleze juhudi zao za kuchangia damu.
Naye Balozi
Najem alisema kuchangia damu ni sehemu ya malengo yake binafsi pamoja na ofisi
yake, hivyo yupo tayari kusaidia kwa namna moja ama nyingine ili kuwasaidia
watu wote wenye uhitaji wa damu nchini Tanzania.
“Nimejiwekea
utaratibu wa kujitolea katika jamii yakiwamo haya mambo ya damu, hivyo pamoja
na kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo pamoja na mliohudhuria kuja kutoa damu,
naomba niwaambie bado nipo tayari kujitolea wakati wowote itakapohitajika,”
Alisema Balozi Najeem.
Awali
Mtendaji Mkuu msaidizi wa TYPF, Swalehe Jabri, aliwashukuru waliojumulika nao
kutoa damu, akisema wamefanya jambo kubwa linalohitaji kuungwa mkono na kila
Mtanzania mpenda maendeleo, akiamini utaratibu huo umelenga kuwasaidia wagonjwa
wenye uhitaji wa damu kwenye hospitali nchini.
No comments:
Post a Comment