Wazazi, walezi wanajamii na wadau mbalimbali wanatarajiwa kukutana kwenye tamasha maalum la taarab lililopewa jina la 'Usiku wa Mswahili' kwa lengo la kukusanya fedha za kuchangia ununuzi wa madawati, linatarajiwa kufanyika usiku wa Ijumaa ya Aprili 24, katika shule ya Tambaza, iliyopo Ilala jijii Dar es Salaam.
"Karibuni katika Usiku wa Mswahili Ijumaa hii ya Aprili 24 ndani ya ukumbi wa Tambaza, kuanzia saa moja usiku. kwa kiingilio cha sh 10,000 na sh 20,000 kwa VIP".
Aidha, mwagwiji wa burudani ya taarab nchini ikiwemo bendi ya Gusa Gusa Min Band na gwiji wa Old Is Gold, Mohd Ilyas watatoa burudani hiyo ambapo pia Malkia wa mipasho nchini, Khadija Kopa naye atakuwapo kukamilisha uhondo wa usiku huo wa Mswahili.
Kwa sasa tayari tiketi zimeanza kuuzwa sehemu mbalimbali ikiwemo Fabak Fashions (Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere), Falcon Restaurant-Lumumba,Hasani Juice-Mtaa wa sukukuu-Big Mayai na kwa Afisa Elimu Msingi,Manispaa ya Ilala.
Tamasha hilo la usiku wa Mswahili linatarajiwa kukutanisha wazazi, walezi na watu mbalimbali wakiwemo wadau wakubwa kwa lengo la kuchangia madawati.