Pages

Pages

Sunday, April 12, 2015

Dr Damas Ndumbaro ashindwa kuhudhuria TFF kusikilizwa rufaa yake

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Kamati ya Rufaa ya Nidhamu - TFF imekutana leo tarehe 12/04/2015 kujadili rufaa No. 1/2014 ya DR. DAMAS  NDUMBARO dhidi ya TFF.

Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto, aliuambia Mtandao huu kuwa Shirikisho hilo la Soka nchini (TFF) iliwakilishwa na Wakili Msomi Emmanuel Muga na Dr. Ndumbaro hakufika wala hakuwakilishwa na wakili wake.

Kufuatia kutofika kwa Dr. Ndumbaro, Kamati, kwa Azimio moja, iliamuru TFF itoe wito mpya na  mpaka tarehe 14/04/2015 uwe umemfikia Dr. Ndumbaro, ukimfahamisha tarehe ya kikao kijacho cha kusikiliza rufaa yake.

No comments:

Post a Comment