Pages

Pages

Friday, April 10, 2015

Maveterani wa Barcelona watua Zanzibar

Rais wa Heshima wa Timu ya Barcelona Kocha Johan Cruyff, akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar alipofika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kikosi cha Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakitokea Arusha , wakiwa Zanzibar kwa Mualiko wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kutembelea Zanzibar kujionea Vivutio vya Utalii na kujionea Vipaji vya Wachezaji Vijana wanaocheza katika timu mbalimbali za Watoto.
Waandishi wa habari za michezo Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuipokea Timu ya Wachezaji wa Wazamani wa Timu ya Barcelona.

Kikundi cha ngoma wakitowa burudani wakati wa ujio wa Wachezaji wa zamani wa timu ya Barcelona Zanzibar. kwa ziara ya siku moja Zanzibar. kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Viongozi wa Vyama vya Mpira Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wakiipokea timu ya Wachezaji wa zamani wa Barcelona walipowasili Zanzibar. 
Ndege ya Serekali ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ikiwa na Wachezaji wa Mastar wa Zamani wa Barcelona wakiwasili Zanzibar kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohemed Shein, na kujionea Vipaji vya Wachezaji wa timu za Watoto katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Bi Shery Khamis akisalimiana na mchezaji nyota wa timu ya wachezaji wa zamani wa Barcelona Kulvert alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja Zanzibar. 
Wachezaji Nyota wa Timu ya Barcelona wakisalimiana na Viongozi wa Vyama vya Michezo Zanzibar baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.










No comments:

Post a Comment