Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA),Bi. Irene Isaka (aliesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na hali
halisi ya sekta ya hifadhi ya jamii nchini,changamoto na mafanikio
wakati wa semina ya siku moja iliyotolewa kwa Wahariri wa Nyombo mbali
mbali vya habari nchini kupitia Jukwaa la Wahariri,iliyofanyika Mwishoni
mwa wiki katika Hoteli ya Oceanic, Bagamoyo.
Mhariri Mkuu wa gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu akiuliza swali mara baada ya uwasilishwaji mada.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA),Irene Isaka akisisitiza jambo juu ya umuhimu wa vyombo vya habari
katika kutoa elimu ya hifadhi ya jamii kwa wananchi.kushoto kwake ni
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini, Absalom Kibanda na kushoto
kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamashishaji wa Mamlaka ya
Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde
– Msika.