Pages

Pages

Friday, December 27, 2013

Malaika bendi wazidi kuchapa mwendo



Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa bendi ya Malaika, Michael Loki, amesema kwamba baada ya kuonyesha makali yao, sasa wanajipanga zaidi kulinda heshima yao kwa kuhakikisha kuwa mashabiki wao wanapata burudani kali.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Loki alisema kwamba vijana wao wapo imara wakiongozwa na Rais wa bendi hiyo, Christian Bellah, hivyo wanaamini wadau wao wataendelea kupata vitu vizuri kutoka kwao.


Alisema kuwa katika shoo zao nyingi walizokuwa wakifanya tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo, mashabiki wamekuwa wakiingia kwa kwa wingi na kuonyesha shauku ya kuburudika.


“Tulikuwa na kiu kubwa ya kuonyesha cheche zetu katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini, hivyo hakuna kitakachotufanya tulale na kuacha wengine wakifanya vyema katika ramani ya muziki huo,” alisema.


Uzinduzi wa bendi hiyo ulifanyika mapema mwezi uliopita katika Ukumbi wa Mzalendo Pub, Kijitonyama, huku ukihudhuriwa na watu wengi waliokwenda kuangalia manjonjo ya vijana wa Malaika.

No comments:

Post a Comment