Pages

Pages

Sunday, December 29, 2013

Twanga kuendeleza moto wake Leaders Club leo jijini Dar es Salaam


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BAADA ya kufanya shoo ya aina yake wilayani Kilosa mkoani Morogoro, Ijumaa na Jumamosi kuwachezesha Mango Garden, bendi ya The African Stars Twanga Pepeta, leo inawapa burudani wapenzi wake katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.



Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, pichani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Hassan Rehan, alisema kuwa vijana wao wapo imara kwa kutoa burudani katika maeneo yao ya kujidai.


Alisema Leaders na Mango Garden ni maeneo ambayo lazima wawepo kika wiki, hivyo wanaamini mashabiki wao wataendelea kupata burudani kamili kutoka kwao.


“Ijumaa tulicheza Kisigino na mashabiki wetu wa Morogoro katika Ukumbi wa Babylone uliopo wilayani Kilosa na kuwaonyesha makali ya Twanga Pepeta,” alisema Rehani.


Baadhi ya wakali wa Twanga Pepeta wanaotamba katika bendi hiyo ni pamoja na Luiza Mbutu, Salehe Kupaza, Grayson Semsekwa, Dogo Rama, Kalala Junior na wengineo.

No comments:

Post a Comment