Pages

Pages

Monday, December 30, 2013

Cindy aleta kicheko Mapacha Watatu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UJIO wa mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu, Catherine Cindy umeleta kicheko kwa viongozi wake, baada ya kuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacota, katikati akiwa na wanamuziki wake, Jose Mara kulia na Khalid Chokoraa kushoto.
 
Cindy aliwasili nchini juzi akitokea nchini Japan, hivyo kusubiriwa kwa hamu na wadau wa bendi hiyo inayoongozwa na Khalid Chokoraa na mwenzake Jose Mara kama wakurugenzi.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mapacha Watatu, Khamis Dacota, alisema kuwa mwanadada huyo ameleta uhai zaidi kutokana na ubora wake jukwaani.
 
“Catherine si mtu wa kawaida na kila mdau wa muziki wa dansi anafahamu uwezo wake, hivyo sisi wote tumefarijika na kurejea kwake,” alisema.
 
Mwanadada huyo ni miongoni mwa vijana wadogo wenye ujuzi wa kucheza na sauti zao, huku makali yake yakitarajiwa kumuweka juu mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.
 

No comments:

Post a Comment