Pages

Pages

Sunday, December 29, 2013

Malaika bandi kuwapa raha Tanga Hoteli leo jijini Tanga


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BENDI iliyokuja kwa kasi katika anga ya muziki wa dansi hapa nchini, Malaika, leo inawapa raha mashabiki wa jijini Tanga, katika Ukumbi uliopo ndani ya Tanga Hoteli.


Safari ya bendi hiyo katika mkoa wa unaotajwa katika sekta ya uhusiano wa kimapenzi ni mwendelezo wa kujitangaza na kujitanua zaidi kwa mashabiki wao wa muziki wa dansi.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa bendi hiyo, Fadhili Mfate, alisema kuwa mashabiki wa jijini Tanga watapata vitu vya aina yake kutoka kwa wanamuziki wenye makali ya kutisha.


“Hii ni safari ya mwendelezo kwa mashabiki wa Tanga ambapo mara baada ya kuzindua bendi yetu tulikuja kujitambulisha kwao.


Tunaamini wote watakaohudhuria shoo wataelewa kwanini tunajitamba kuwa tumesheheni vijana wenye uwezo wa juu kisanaa,” alisema Mfate.


Malaika ipo chini ya Mkurugenzi wake Michael Loki, ambapo Rais wa wanamuziki ni Christian Bellah, anayeheshimika mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa nchini.

No comments:

Post a Comment