Pages

Pages

Friday, December 27, 2013

Mpira Pesa wazidi kumchulia mwenyekiti wao wa Simba, Aden Rage


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

MWENYEKITI wa Tawi la Mpira Pesam Ustadh Masoud, amesema moto wa kutokuwa na imani na mwenyekiti wao Ismail Aden Rage umesambaa nchi nzima, kutokana na kiburi anachoonyesha mwenyekiti wao.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Masoud alisema kwamba Rage ni mbishi asiyependa kusikiliza ushauri wa mtu yoyote, huku akijidanganya kwamba ni Mpira Pesa tu wasiyokuwa na imani naye.


Alisema mara kadhaa Rage anatushutumu sisi Mpira Pesa, ila wakati huu kila mtu anayeipenda Simba hafurahishwi na mwenendo wa mwenyekiti wetu, ndio maana hata ushauri aliyopewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya kuitisha Mkutano ameshindwa kuutekeleza.


“Sio Mpira Pesa tu wanayeumizwa na mwenendo wa mwenyekiti wetu Rage, maana nchi nzima sumu yake imezagaa, hivyo nadhani ni wakati wake kukaa na kusikiliza malalamiko ya wanachama wake,” alisema.


Sakata la mgogoro wa Rage ndani ya klabu ya Simba unazidi kushika kasi, jambo ambalo lilisababisha TFF wao wamtake aitishe mkutano kwa ajili ya kumaliza tofauti zake na wanachama wake, ingawa ushauri huo haujafanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment