Pages

Pages

Sunday, December 29, 2013

Kaseba achekelea kumdunda Alibaba


Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Japhet Kaseba, amesema ushindi wake dhidi ya Ramadhan Alibaba, ulitokana na maandalizi yake pamoja na dhamira ya kuonyesha makali yake.


Pambano lao lilimalizika katika raundi ya nne, baada ya Alibaba kushindwa kuendelea, hivyo mwamuzi kumpa ushindi Kaseba.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema kuwa anaamini maandalizi yake yatazidi kumuweka katika nafasi nzuri ya kutangaza makali yake kwenye masumbwi.


Alisema kuwa makali yake katika mchezo wa ngumi yanampa imani kuwa ataendelea kuwa juu kiasi cha kutoa kichapo kwa kila bondia atakayekutana naye ndani ya ulingo.


“Sijabahatisha kucheza na kumpiga Alibaba, maana nimedhamiria kuonyesha umwamba wangu kwa kila atakayepanda na mimi ulingoni,” alisema Kaseba.


Hata hivyo, Alibaba mwenyewe alisikika akilaumu ushindi wa Kaseba akisema mara kwa mara alikuwa akimchezea rafu, hivyo ameshinda kwa hila na si uwezo kama anavyojigamba.

No comments:

Post a Comment