Pages

Pages

Monday, December 30, 2013

Msanii auelezea wimbo wa Safari ya Tanga

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Ahmad Salum ama (Mady Salu), amesema kwamba ili aweze kushiriki katika Tamasha la Handeni Kwetu ilimlazimu aingie Studio kurekodi wimbo uliokwenda kwa jina la ‘Safari ya Tanga’.
 
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mady Salu alisema kwamba hatua hiyo ilisababishwa na uchu wake wa kupania kupanda katika jukwaa la tamasha lililofanyika kwa mara kwanza.
 
Alisema mara nyingi wasanii wachanga wamekuwa wakipata nafasi hiyo mara chache mno, hivyo nafasi yake ya kupangwa kuwapo katika tamasha hilo kulimfanya ajiandaye vizuri.
 
“Nisingepata nafasi ya kushiriki ningeumia kwakuwa niliambiwa namna gain ya kufanya ili niweze kufanya vyema katika tamasha.
 
“Tamasha lilihusu utamaduni, hivyo kitendo cha kurekodi wimbo wangu wa Safari ya Tanga hakika ulinitangaza vizuri na kuonyesha pia shauku ya kutangaza kipaji changu katika muziki wa kizazi kipya,” alisema.
 
Mady Salu aliwahi kuwapo katika kundi la Ngovita Clew lililotambulisha wimbo wa Maisha Miangaiko, ambalo baadaye liligawanyika.

No comments:

Post a Comment